Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mnoga anavizia timu za League One

MNOGA Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na Salford uliomalizika Mei 31 mwaka huu na inaelezwa Mnoga alikataa kuongeza mkataba mpya na timu hiyo ili kutafuta changamoto nyingine katika ngazi ya juu zaidi ya soka la England.

BAADA ya kumaliza mkataba wake na Salford City ya England, inaelezwa beki wa Mtanzania, Haji Mnoga kuna timu mbili kutoka League One zimeanza kumfuatilia.

Nyota huyo alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na Salford uliomalizika Mei 31 mwaka huu na inaelezwa Mnoga alikataa kuongeza mkataba mpya na timu hiyo ili kutafuta changamoto nyingine katika ngazi ya juu zaidi ya soka la England.

Mnoga, mwenye umri wa miaka 24 sasa ni mchezaji huru, hali inayompa nafasi ya kumalizana na klabu yoyote baada ya kumaliza majukumu yake na Salford City inayoshiriki Ligi Daraja la Nne (League Two).

Taarifa zinaeleza kuwa beki huyo alipewa nafasi ya kuongeza mkataba na Salford City, lakini aliamua kukataa ofa hiyo akiamini ana uwezo wa kucheza katika klabu inayoshiriki League One, ambayo ni daraja la tatu la soka nchini England.

MNOGA Pict

“Ofa waliokuwa wamemuwekea ilikuwa ndogo tofauti na matakwa yake lakini pia kilichochangia zaidi baada ya timu kushindwa kupanda daraja na kwa sasa Mnoga anatamani kucheza ligi za juu England,” kilisema chanzo cha karibu na mchezaji huyo na kuongeza

“Kuna ofa kubwa zipo na timu kutoka League One hivyo anaangalia uwezekano wa mojawapo kwa hiyo kwa sasa yupo kwenye mchakato wa kuzichambua.”

Akiwa Salford City, Mnoga alicheza jumla ya mechi 33 za mashindano yote na kujitengenezea nafasi ya kwanza ndani ya kikosi hicho kutokana na kiwango chake cha utulivu na uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali za ulinzi.

MNOGA Pict

Kabla ya mkataba wake kumalizika, kiwango chake kilivutia klabu kadhaa za England. Miongoni mwa timu zilizowahi kuonyesha nia ya kumhitaji ni Rotherham United, ambayo ilitajwa kuweka mezani dau la pauni 250,000 kwa ajili ya usajili wake, pamoja na Lincoln City, iliyokuwa ikifuatilia maendeleo yake.

Hata hivyo, hadi sasa hakuna klabu iliyotangaza rasmi kufikia makubaliano ya kumsajili, huku Mnoga akiendelea kutathmini ofa zinazoweza kumpa nafasi ya kucheza katika kiwango cha juu zaidi.

Beki huyo aliyewahi kupita kwenye akademi ya Portsmouth na kupata nafasi katika timu za vijana za England kabla ya kuamua kuitumikia Tanzania, ameonyesha kiwango kizuri kilichomfanya kuwa sehemu muhimu ya kikosi hicho katika kampeni ya msimu huu.

Akicheza kwa misimu miwili Salford, msimu huu Mnoga alicheza mechi 25 za ligi kwa dakika 1697 akitoa mchango wake katika safu ya ulinzi ya Salford City iliyokuwa ikisaka kurejea League One kwa mara ya kwanza tangu kushuka daraja.