Mkude apiga tano Simba, Yanga

KIUNGO Jonas Mkude ameingia kwenye rekodi akiwa mchezaji ambaye timu yake ilishinda kwa bao tano kwenye mechi ya dabi ya Kariakoo.
Mkude alianza kufanya hivyo Mei 6, 2012 akiwa na Simba wakiikanda Yanga mabao 5-0 na leo tena akiwa na Yanga wameshinda 5-1.
Kiungo huyo ambaye ameingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mudathir Yahya amekuwa mchezaji wa kwanza kuandika rekodi hiyo.
Mkude ambaye amesajiliwa msimu huu kwa mkataba wa mwaka mmoja akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika Simba ametumia dakika mbili tu kuandika rekodi hiyo akiingia dakika ya 88.