Mkongwe wa Yanga aipeleka Bandari nusu fainali

Muktasari:

Tulikuwa na malengo, kwanza ni kushinda mechi hii ya kwanza ili kuwapa wachezaji wangu kujiamini zaidi kwani ukiangalia kikosi changu kina wachezaji wengi vijana..

Dar es Salaam. Kocha wa Bandari ya Kenya,Bennard Mwalala amesema  sasa anaweza kutoka kifua mbele na hana hofu ya  kukutana na yeyote kwenye mashindano ya Kombe la SportPesa.
Mwalala alisema mechi ya leo dhidi ya Singida United ndio ilikuwa ngumu kwake na baada ya kupata ushindi hana tena hofu na mechi nyingine zinazofuata kwani hata akikutana na Simba  au Yanga kwake poa tu.
"Nilikuwa na hofu na mechi hii kwani ndio ilikuwa ngumu kwetu kwa sababu ni mechi ya kwanza lakini sasa naamini wachezaji wangu hawana wasiwasi tena.
"Tulikuwa na malengo,kwanza ni kushinda mechi hii ya kwanza ili kuwapa wachezaji wangu kujiamini zaidi kwani ukiangalia kikosi changu kina wachezaji wengi vijana.
"  Ushindi huu umetupa morali na  tunaweza kufanya vizuri zaidi na kufika hata fainali" alisema Mwalala.
Aliongeza"Sasa hivi hata nikikutana na Simba au Yanga  poa tu kwa sababu itawafanya vijana wangu kupata uzoefu na kuona jinsi timu hizo zilivyo na mashabiki wengi.