Mkojani: Ubora wa Simba utailiza Yanga!

Muktasari:

MSANII mwenye vichekesho vyake mjini, Abdallah Mohamed 'Mkojani' hajaficha namna Simba inavyompagawisha na ametaja anachokitarajia mechi ya watani wa jadi Yanga siku ya Jumamosi ya Mei 8, mwaka 2021 kwamba itampa kicheko kutokana na ubora wa wachezaji wa timu hiyo.

Mkojani ni Simba damu, ameliambia Mwanaspoti Online, leo Jumatatu ya Mei 3 kwamba Simba ipo kwenye kiwango cha juu, ambacho hakiwapi shaka kupata matokeo ya kuwapa kicheko kwamba ni tofauti na upande wa pili ambao wanaungaunga.

"Hii ni Simba ya viwango vingine, imeanza kuonyesha ubora wake Caf sembuse ligi ya ndani, najua ushindani mkali ambao unakuwepo mechi ya dabi, lakini kwa namna kocha Didier Gomes alivyo na mbinu anatupa nguvu ya kutamba mtaani," amesema na ameogeza kuwa;

"Simba ina wachezaji wenye ushindani wa namba wenyewe kwa wenyewe, hilo linasaidia kumpa uhuru kocha wa kutokuwa na kikosi kinachozoeleka na hilo litafanya wawe na ubora dhidi ya Yanga ingawa najua wazi kwamba mechi itakuwa ngumu," amesema.

Amewahamasisha mashabiki wa Simba, kuungana kwa pamoja kwenda kuwashabikia wachezaji wao kuhakikisha wanapata morali ya kujituma, ili kuwapa furaha wanayoitaka.

"Mechi za watani wa jadi zinatokea mara mbili kwa mwaka na kwa jinsi ambavyo zina ushindani mkali na maumivu pamoja na furaha kwa timu inayoshinda.