Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mke wa Tom Olaba awalilia Watanzania

OLABA Pict

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Kenya, mke wa kocha huyo, Elizabeth Olaba alisema kwa sasa Olaba matibabu yake yamekuwa ghali hivyo, anawaomba wadau mbalimbali wa soka kutoka Tanzania, Kenya na Uganda kumsaidia ili kutatua changamoto hiyo.

KOCHA mkuu wa zamani wa Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting za Tanzania, Mkenya Tom Olaba anasumbuliwa na maradhi ya kupooza mwili baada ya kufanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo, huku mkewe akiomba misaada mbalimbali kwa ajili ya matibabu yake.

Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Kenya, mke wa kocha huyo, Elizabeth Olaba alisema kwa sasa Olaba matibabu yake yamekuwa ghali hivyo, anawaomba wadau mbalimbali wa soka kutoka Tanzania, Kenya na Uganda kumsaidia ili kutatua changamoto hiyo.

“Kwa sasa hawezi kufanya chochote, huwezi amini hata simu ya mkononi ukimpa ashike inadondoka chini, nashukuru baadhi ya wadau wa Kenya wanamtembelea na kutoa misaada mbalimbali, jambo ambalo kwetu linatupa faraja sana,” alisema Elizabeth.

Elizabeth alisema kwa sasa Olaba anaendelea na matibabu ya tiba ya mwili (Physiotherapy) anayoendelea nayo kwa wiki mara mbili, ingawa shida ni gharama kwa sababu kwa siku moja anatumia kiasi cha Ksh30,000 ambayo kwa Tanzania ni Sh 625,991.

Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Kenya kinachojulikana kwa jina la The Sports Journalists Association of Kenya (SJAK), kupitia kwa Rais wake, James Waindi akiwa sambamba na kocha wa zamani wa Fountain Gate, Robert Matano, walimtembelea kocha huyo na kutoa misaada mbalimbali ikiwamo vyakula.

Akizungumza na Mwanaspoti, Waindi alisema kama Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Kenya wanatambua mchango wa kocha Olaba, ndio maana walitumia fursa ya kumtembelea na kugawa misaada mbalimbali kwa lengo la kuthamini mchango wake.

Olaba aliyeifundisha timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars mwaka 2006, kabla ya kocha wa zamani wa Tusker, Jacob ‘Ghost’ Mulee kurithi mikoba yake, kwa sasa hafanyi chochote zaidi ya kutembelea kiti cha magurudumu yaani ‘wheelchair’.

Pia, Olaba alikuwa ni msaidizi wa aliyekuwa kocha mkuu wa Harambee Stars, raia wa Ujerumani marehemu Reinhard Fabisch mwaka 1997, huku mtaalamu huyo anayesifika kwa mbinu uwanjani akiwahi kuifundisha AFC Leopards ya kwao Kenya mara mbili.

Ziara hayo ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Kenya, ilimjumuisha pia na aliyekuwa kocha wa kikosi cha Fountain Gate ya Tanzania, Mkenya Robert Matano ambaye hivi karibuni aliachana na timu hiyo kwa makubaliano ya pande mbili.