Mgunda: Tunarudi kibabe sana

BAADA ya mapumziko ya siku mbili kikosi cha Simba jana kilirejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City huku Kocha mkuu wake, Juma Mgunda akisisitiza kuendelea walipoishia na watakiwasha kwa nguvu kubwa.

Mgunda ambaye anakaimu nafasi hiyo baada ya kondoka kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Zoran Maki alisema: “Nilitoa mapumziko ya siku mbili Jumatatu na Jumanne, tunaendelea na mazoezi na wachezaji wote mbao hawajapata nafasi ya kuitwa kwenye vikosi vyao vya timu ya taifa hakuna mchezaji aliyeruhusiwa nje ya wale walioenda kwenye mjukumu ya kutumikia Mataifa yao.

“Kipindi hiki ambacho sipo na kikosi kamili wachezaji niliobaki nao nitahakikisha nawafanyisha mazoezi ya kuweka miili yao sawa na masahihisho kulingana na makosa yaliyotekea kwenye mechi zilizopita.”

“Ili kuendana na kasi ni kuhakikisha tunapata matokeo kwenye kila mchezo, tunatarajia kuendelea tulipoishia sio rahisi lakini kumejipanga kwaajili ya ushindani,” alisema na kuongeza kila timu wanayokutanana nayo ni bora.

“Kila kocha ana mbinu zake na wachezaji kwa asilimia kubwa wamebadilika ni kweli Simba hawakupata matokeo dhidi ya Mbeya City haina maana kwamba hata msimu huu itakuwa hivyo hivyo kuna mechi msimu uliopita walishinda mabao zaidi ya matatu na msimu huu huenda wakashindwa kufanya hivyo.”

Mchezo namba 37 kati ya Mbeya City na Simba uliopangwa kuchezwa Septemba 28 saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, sasa utapigwa Novemba 23 kwenye Uwanja huo na muda huo huo.

Akizungumzia mashindano ya CAF, alisema: “Ratiba tumeiona wapinzani wetu tumeshawafahamu tunajiandaa pia kuhakikisha tunaanza vyema ugenini kama tulivyopangiwa ili kuja kumaliza nyumbani, lengo ni kuvuka hatua hii pia ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kutinga hatua ya makundi.”

“Ligi ya Mabigwa Afrika ili uwe na uhakika wa kufanya vizuri ni hatua yoyote ile ni lazima timu iwe na uwezo wa kupata matokeo ugenini au hata bao ambalo linaweza kuwa na faida nyumbani ikitokea ukashindwa kupata matokeo mkatoka sare na wapinzani tumedhuhudia hilo kw Geita Gold ambao wameruhusu nyavu zao kutikiswa nyumbani na kutoa faida kwa wapinzani wao.”

Alisema kushinda ugenini kunapunguza presha kwenye mchezo wa nyumbani na kuifanya timu kuchez kwa hari nzuri yenye tija ya kupata matokeo ambayo yatawafanya wasonge hatua inyofuata.