Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgore amtangazia vita Diarra

VITA ya kulinda lango Ligi Kuu Bara imetawaliwa na makipa wa kigeni, ambao hadi sasa wamefanya vizuri na kuwabwaga wazawa, lakini Daniel Mgore wa Dodoma Jiji amewapa ushindani na kuendelea kufukuzana nao, huku akitamba kuwapa changomoto na kuisaidia timu yake kumaliza katika nafasi za juu.

Zikiwa zimechezwa raundi tisa za ligi hiyo, tano bora ya makipa ambao hawajaruhusu mabao kwenye michezo mingi imetekwa na wageni, kinara Mingeria John Noble wa Tabora United, akiwa na clean sheet tano, akifuatiwa na Djigui Diarra (4), huku Lay Matampi (Coastal Union) na Mghana Idrisu Abdulai wa Azam FC na Mgore kila mmoja ana tatu.

Umahiri wa Mgore umeisaidia Dodoma  kushika nafasi ya nne hadi sasa katika ligi

Akizungumza na Mwanaspoti, Mgore alisema kujiamini, kumuomba Mungu na kupambana ndiko kumemfanya awe bora mpaka sasa, huku akidai kushindana na makipa mahiri kama Diarra na Noble kunampa nguvu ya kujituma zaidi.