Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgaya atamani makubwa Coastal

Mgaya Pict

Muktasari:

  • Kabla ya kujiunga na Coastal nyota huyo aliichezea Fleetwoods United FC, inayoshiriki Ligi Daraja la Pili UAE.

STRAIKA mpya wa Coastal Union, Ally Mgaya amesema anatamani kufanya makubwa akiwa katika kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Juma Mwambusi.

Kabla ya kujiunga na Coastal nyota huyo aliichezea Fleetwoods United FC, inayoshiriki Ligi Daraja la Pili UAE.

Nyota huyo alimaliza mkataba wa miaka miwili hivi karibuni na kabla ya kucheza Falme za Kiarabu aliwahi kutumikia Coastal Union ya vijana U-20 msimu wa 2020/21.

Akizungumza na Mwanaspoti baada ya kutambulishwa na Wanamangushi, Mgaya alisema anatamani kufanya vziuri na kupata nafasi mbele ya kocha Juma Mwambusi.

Akizungumzia ushindani ndani ya kikosi hicho alisema anafahamu ubora wa wachezaji lakini kama mchezaji kazi yake ni kuonyesha uwezo wa kufunga.

"Nilicheza mwanzo lakini timu za vijana nimerudi sasa Ligi Kuu natamani kupata nafasi kikosi cha kwanza na kuonyesha uwezo wangu wa kufunga magoli," alisema Mgaya.