Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam, Lawi tayari kimeeleweka

Muktasari:

  • Mmoja wa viongozi wa timu hiyo akizungumza na gazeti hili jana,  alisema ni kweli mchezaji huyo tayari ameshatia saini mkataba wa kuichezea Azam kwa miaka miwili kuanzia msimu ujao.

AZAM FC ni kama imepindua dili la vigogo waliokuwa wakimsaka beki wa Coastal Union, Lameck Lawi baada ya kuelezwa kwamba imetia mkono na kumalizana na beki huyo wa kati ili avae uzi wa Wanalambalamba kwa msimu wa 2025-2026.

Mmoja wa viongozi wa timu hiyo akizungumza na gazeti hili jana,  alisema ni kweli mchezaji huyo tayari ameshatia saini mkataba wa kuichezea Azam kwa miaka miwili kuanzia msimu ujao.

Awali, Simba msimu uliopita ilitangaza kumsajili Lawi kwa mkataba wa miaka mitatu, lakini mambo hayakuenda sawa dhidi ya timu iliyokuwa inammiliki (Coastal) hadi ikafikia hatua ya kupelekana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Mkataba wa Lawi ulimalizika mwishoni mwa msimu ulioisha, hivyo Simba ilikuwa inasubiri kumchukua akiwa huru, ambapo tayari imewahiwa na Azam iliyo hatua za mwisho kumalizana naye.

Taarifa za ndani kutoka Azam zinaeleza lengo la kumsajili Lawi ambaye atakwenda kupambania namba na mabeki wa kigeni Yeison Fuentes kutoka Colombia na Yoro Diaby ni kuo-ngeza nguvu kama mzawa.

Kwa beki mzawa anayecheza nafasi hiyo Azam ni Abdallah Kheri aliyekuwa anacheza Pamba kwa mkopo, ambapo uongozi utatathmini alichokifanya kama kinaweza kikaongeza nguvu au la.

“Azam ipo katika maboresho ya wachezaji kwa maana wapo wanaosajiliwa na wengine wanaondoka mfano mzuri ni mshambuliaji ambaye kamaliza mkataba, ameaga Gibril Sillah. Lazima atatafutiwa mbadala wake. Ukiachana na hilo pia anatafutwa kocha mpya baada ya kuachana na  Rachid Taoussi,” kilisema chanzo hicho kutoka ndani ya timu hiyo.