Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mfungaji Bora ZPL azigonganisha tatu Bara

MFUNGAJI Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo aliyemaliza msimu wa 2025-2026 akifanikiwa kufunga mabao 21 ikiwemo hat trick iliyoipa KVZ ubingwa siku ya mwisho wa msimu wakiifunga Kipanga 4-0, amesema mazungumzo bado yanaendelea.

MSHAMBULIAJI wa KVZ, Michael Joseph aliyeibuka kinara wa ufungaji katika Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) msimu wa 2025-2026, amezivutia timu tatu za Ligi Kuu Bara ambazo ni Namungo, Coastal Union na Pamba Jiji.

Mshambuliaji huyo aliyemaliza msimu wa 2025-2026 akifanikiwa kufunga mabao 21 ikiwemo hat trick iliyoipa KVZ ubingwa siku ya mwisho wa msimu wakiifunga Kipanga 4-0, amesema mazungumzo bado yanaendelea.

“Mazungumzo yanaendelea, lakini hakuna ambayo imefikia muafaka,” amesema mshambuliaji huyo.

Joseph aliwashukuru makocha wake kwa kuwa na mchango mkubwa kwake hadi kufikia nafasi hiyo ya kuibuka mfungaji bora.

Mshambuliaji huyo ambaye msimu wa 2025-2026 katika Ligi Kuu Zanzibar alicheza kwa dakika 2320, idadi ya mabao 21 aliyofunga na kumpa tuzo ya ufungaji bora, ni sawa na aliyofunga Abdalla Iddi ‘Pina’ msimu wa 2024-2025 akiwa Mlandege ambaye pia alikuwa mfungaji bora. Joseph pia msimu huu ametoa asisti nane na kumfanya kuhusika kwenye mabao 29 akicheza mechi 29.

Msimu uliopita, Joseph alimaliza ligi nafasi ya pili kwa ufungaji akiwa na mabao 17 akicheza mechi 21, huku akisisitiza kuwa msimu huo hakuanza vizuri.

Aliliambia Mwanaspoti kuwa, siri ya mafanikio hayo msimu huu ni kuongeza nguvu na juhudi ya kuhakikisha anafikia malengo yake na timu.

“Baada ya kumaliza nafasi ya pili msimu uliopita niliongeza nguvu nilipoishia na hatimaye nimefanikiwa kuwa mfungaji bora msimu huu,” amesema.

Alieleza, kilichompa furaha zaidi ni kufunga mabao manne yaliyoipa ubingwa timu hiyo.