Mechi ya Yanga, JKU ulinzi mkali Gombani

Muktasari:
- Yanga iliingia fainali kwa kuifunga Zimamoto kwa penalti 3-1 katika mechi dhidi ya nusu fainali ya pili mashindano ya Kombe la Muungano uliopigwa kwenyeb Uwanja wa Gombani Pemba na JKU iliingia fainali kwa kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Azam.
SAA chache kabla ya Yanga kuvaana na JKU leo Alhamisi katika pambano la fainali ya Kombe la Muungano, kamishna Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Abdallah Hussein Mussa amesema ulinzi utaimarishwa katika mechi hiyo italayopigwa kwenye Uwanja wa Gombani uliopo visiwani utakaopigwa kuanzia saa 1:15 usiku.
Yanga iliingia fainali kwa kuifunga Zimamoto kwa penalti 3-1 katika nusu fainali ya pili michuano hiyo, huku JKU ikiingia fainali kwa kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Azam.
Kwa kutambua umuhimu wa mchezo huo, Jeshi la Polisi limesema limejipanga vizuri kuhakikisha wananchi, wanachama, mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu wanashiriki katika mchezo huo kwa amani na salama.
"Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vyingine vya ulinzi na usalama linahakikisha linazuia matukio ya kihalifu ya aina yoyote yanaweza kujitokeza kabla na baada ya mchezo," amesema Kamanda Abdallah.
Kamanda huyo, amesema mechi kubwa kama hizo zimekuwa na matukio ya uhalifu ikiwemo wizi wa simu, fedha na vyombo vya moto, hivyo amehakikisha kuwa ulinzi utakuwepo katika maeneo yote kwa lengo la kudhibiti vitendo hivyo.
Kamanda huyo, ametoa wito kwa madereva wa vyombo vya moto kutotumia michezo hiyo kuvunja sheria za usalama wa barabarani watakaokiuka sheria watachukuliwa sheria.
Yanga itashuka uwanjani ikisaka taji la saba la michuano hiyo iliyoasisiwa mwaka 1982 na kuchezwa hadi 2002 kabla ya kusimama tangu 2003 na kurejeshwa mwaka jana na Simba kubeba ubingwa kwa kuifunga Azam FC kwa bao 1-0.
Kwa JKU itakuwa ikisaka taji la kwanza, kwani ni mara ya kwanza kutinga hatua hiyo.