Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mboto ampa saluti Dube

MSANII wa vichekesho, Mboto Haji maarufu kama Mboto, amesema bao alilofunga straika wa Azam FC, Prince Dube linastahili pongezi na kwamba kufungwa Yanga sio dhambi, bali  ni mojawapo ya matokeo matatu yaliopo katika mpira wa miguu.

Mboto ambaye ni shabiki wa Yanga lialia, ameliambia Mwanaspoti online, leo Jumatatu ya Aprili 26, mwaka 2021 kwamba bado ana imani na ubingwa na wachezaji wa timu hiyo kwamba watapambana kupata matokeo katika mechi zilizosalia.

"Kwanza nampongeza Dube ni straika mpambanaji, tangu mechi imeanza alikuwa anaonyesha kuwa na njaa ya mabao, ukiachana na hilo kafunga bao la akili, huo ndio mpira na watu lazima wajue kwamba Yanga kufungwa sio dhambi bali ni moja ya matokeo matatu, ushindi, sare na kufungwa," amesema.

Ameongeza kuwa mechi yao na Azam FC imepita, kilichobakia ni kuangalia namna ya kuwatia moyo wachezaji kupambana kwa michezo iliobakia ili waweze kumaliza ligi ya msimu huu kibabe.

"Hakuna haja ya mashabiki wa Yanga tuanze kutembea kinyonge, huu ni mpira hata hao Simba wanaweza wakafungwa vilevile ngoma ikawa droo, tunachotakiwa kuangalia ni jinsi ya kumaliza kwa kishindo," amesena.
mwisho.


Dube atoa neno
MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Prince Dube amesema licha ya kufunga bao zuri dhidi ya Yanga, kilichomfurahisha ni kuipa timu yake pointi tatu katika mechi iliyokuwa na ushindani mkali, uliotoa burudani kwa mashabiki wao.

Dube amesema ni kiu ya kila straika kufunga mabao kwasababu ndio kazi inayowaweka kwenye timu walizopo, akifafanua kwamba amepata faraja baada ya kuifunga Yanga ambayo iliwafunga mzunguko wa kwanza kwenye Uwanja wa Chamanzi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

"Hakuna mshambuliaji asiyependa kufunga, ndio maana mechi yetu na Yanga ilikuwa ngumu na yaushindani, lakini tunashukuru kwa upande wetu tumefanikisha malengo yetu sasa tunaangalia  mechi zilizopo mbele yetu hatuwezi kulewa sifa wakati tuna kazi ngumu sana mbele yetu," amesema  na ameongeza kuwa,

"Unajua mpira ni dakika 90, hilo linatuaminisha kwamba Azam FC bado tuna nafasi ya kupambania ubingwa hadi dakika ya mwisho, ndio maana tunatamani kufunga kila mechi zilizopo mbele yetu tuone baada ya hapo tutavuna nini," amesema.

Mbali na hilo amesema ushindani uliopo katika nafasi ya kufunga mabao ni mkubwa, lakini anachokiangalia nikuweka malengo na manufaa ya timu mbele, mengine yatajiweka sawa mbele ya safari.
"Narudia tene ni ndoto ya kila straika kuona anafunga bao, lakini lazima kila mchezaji atangulize maslahi ya timu kwasababu kila ina malengo yake ya msimu," amesema.
mwisho.