Mbosso na Aviola laivu Jangwani

Muktasari:
- Yanga imemvuta Mbosso kuwa msanii maalum atakayetumbuiza katika kilele cha paredi la ubingwa wakati timu hiyo itakapomalizia msafara wa kutembeza mataji matano iliyotwaa msimu huu.
Katika makao makuu ya Yanga hapatoshi, baada ya klabu hiyo kumshusha msanii Mbwana Kilungi maarufu kwa jina la Mbosso Khan.
Yanga imemvuta Mbosso kuwa msanii maalum atakayetumbuiza katika kilele cha paredi la ubingwa wakati timu hiyo itakapomalizia msafara wa kutembeza mataji matano iliyotwaa msimu huu.
Yanga imeshatua jijini Dar es Salaam, ikitokea Zanzibar ilipotwaa taji la tano la ubingwa wa Kombe la Shirikisho jana baada ya kuichapa Singida Black Stars kwa mabao 2-0.
Mbosso anayetamba na nyimbo mpya mbili za Power na Aviola atatumbuiza makao makuu ya klabu hiyo wakati kikosi cha timu hiyo kitakapofika hapo.
Yanga inautumia wimbo wa Aviola kama kijembe kwa watani wao ambao wamekosa mataji msimu huu.
Yanga imechukua ubingwa wa Kombe la Toyota, Ngao ya Jamii, Kombe la Muungano, Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho.