Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbao yaikamia Simba

Muktasari:

  • Kocha huyo Mrundi alisema Mbao inahitaji ushindi, hivyo hakuna sehemu nyingine ya kuupata tofauti na kwa Simba na mechi nyingine zilizobaki.

Mwanza. Kocha Mkuu wa Mbao FC, Ettiene Ndayiragije amesema wanahitaji kulipa kisasi dhidi ya Simba kwa kuhakikisha wanashinda nyumbani.

Mbao itakuwa mwenyeji wa Simba Aprili 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kocha huyo Mrundi alisema Mbao inahitaji ushindi, hivyo hakuna sehemu nyingine ya kuupata tofauti na kwa Simba na mechi nyingine zilizobaki.

“Mchezo utakuwa mgumu, wenzetu wanataka pointi na sisi tunahitaji, hatuna presha yoyote tumejiandaa kiushindani nahitaji kulipa kisasi kwenye mchezo huu,”alisema Ettiene.

Mrundi huyo alisema amewaandaa vijana wake kisaikolojia na anaamini hawatomuangusha kwenye mchezo huo.