Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayele, Saido wagawana kiatu

Fiston Mayele wa Yanga na Saido Ntibazonkiza kutoka Simba wote wamepewa tuzo ya mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara 2022/23.

Mayele na Saido kila mmoja alifunga mabao 17 hivyo Kamati ya Tuzo ilikaa na kuangalia kanuni zinaelekezaje wachezaji wanapofunga mabao hivyo kila mmoja kupata tuzo.

Mayele ambaye ameenda kwenye majukumu ya timu yake ya Taifa DR Congo tuzo yake ilipokelewa na mke wake ambaye aliwashukuru kwa tuzo hiyo.

Hata hivyo Mayele amezungumza akiwa kwenye kambi ya timu ya Taifa akisema; "Nashukuru wote kuanzia viongozi, wachezaji, mashabiki walionipa sapoti kubwa.

"Hata mechi ya mwisho nililazikika kucheza huku nikipewa sapoti kubwa sana, natamani ningekuwepo ila nipo kwenye majukumu ya timu ya Taifa," amesema Mayele

Saido pia amewashukuru uongozi wa Geita Gold na Simba SC kumsaidia kubeba kiatu hicho.