Mayele afuata tuzo yake Congo

MSHAMBULIAJI kinara wa Ligi Kuu Bara, Fiston Mayele ameifuata tuzo yake DR Congo ambayo inatarajiwa kutolewa Januari 7 mwaka huu.

Mayele ameondoka jioni hii kuelekea nchini kwao ambapo safari yake ni maalum kwaajili ya kushughulikia hati yake ya usafiri lakini pia ameweka wazi kuwa atasubiri na tuzo yake.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mayele amesema amefurahia kupewa heshima na nchi yake kwa kumchagua kuwa mchezaji bora wa nchi yake.

“Ninafuraha na nathamini hiki walichokifanya wananifanya niongeze juhudi zaidi ya kupambana nikijua kunawatu wananifuatilia na kuthamini kile ninachokifanya,” amesema na kuongeza;

“Nitakuwa huku hadi Januari 8 ambapo nitaanza safari ya kurudi nchini Tanzania kuungana na timu kwaajili ya kuendelea na majukumu ya timu.”