Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayanga aita 24 kuikabili Benin

Muktasari:

  • Taifa Stars itacheza mechi ya kirafiki ya kwanza ugenini tangu Mayanga achukue jukumu la kuinoa timu hiyo.

Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza kikosi c ha wachezaji 24, kitakachoingia kambini mwezi ujao kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Benin.

 Taifa Stars itacheza mechi hiyo ya kirafiki ugenini Novemba 11, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kocha Mayanga achukue jukumu hilo.

Tanzania katika mchezo uliopita wa kirafiki dhidi ya Malawi ililazimisha sare ya bao 1-1 matokeo yaliyoiporomosha kwa nafasi 11 katika viwango vya Fifa hadi kufikika 136.

Wakati Tanzania ikiwa ya 136, katika viwango hivyo wapinzani wao Benin ipo nafasi ya 79 katika ubora wa Fifa na mwezi uliopita walipanda kwa nafasi tisa (9).

Katika kikosi hicho kocha Mayanga ameita wachezaji watatu wa kikosi cha timu ya vijana na wazoefu 21 tayari kwa mchezo huo.

Kikosi cha Stars kinaundwa na  Makipa ni Aishi Manula(Simba), Ramadhani Kabwili (Yanga) na Peter Manyika (Singida United).

Mabeki  ni Gadiel Michael (Yanga), Erasto Nyoni (Simba), Boniface Maganga (Mbao FC), Nurdin Chona(Tanzania Prisons), Abdi Banda (Baroka FC, Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Yanga) na Dickson Job (Mtibwa Sugar).

Viungo ni Himid Mao (Azam), Hamis Abdallah (Sonny Sugar, Kenya), Mzamiru Yassin (Simba), Raphael Daud (Yanga),Simon Msuva (Difaa El Jadidi, Morocco), Shiza Kichuya (Simba), Farid Mussa (Tenerife, Hispania), Abdul Hilal (Tusker, Kenya), Mohammed Issa (Mtibwa Sugar) na Ibrahim Ajib (Yanga).

Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Mbaraka Yusuph (Azam), Elias Maguri (Dhofar, Oman) na Yohana Mkomola (Etoile du Sahel, Tunisia).