Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matola ageuka ‘lulu sokoni’


WAKATI hatma ya benchi la ufundi la Simba ikiendelea kuwa gumzo kuelekea mwisho wa msimu, taarifa zinaeleza kocha msaidizi wa timu hiyo, Seleman Matola ameanza kuvutia macho ya Polisi Tanzania ambayo ipo kwenye hesabu za kujenga kikosi na benchi imara endapo itafanikiwa kupanda Ligi Kuu Bara mwishoni mwa msimu.


Matola ni mmoja wa makocha waliodumu kwa vipindi tofauti ndani ya Simba akiwa sehemu ya benchi la ufundi tangu mwaka 2018 na ameshiriki katika mafanikio mbalimbali ya klabu hiyo ndani na nje ya nchi.

Uzoefu wake kwenye mazingira ya Ligi Kuu Bara umeendelea kumfanya mmoja wa makocha wanaotajwa karibia kwenye timu nyingi za Ligi Kuu Bara kwa sasa.

Matola ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba amewahi kutajwa kuwa anatakiwa na Geita Gold ambayo imeshapanda daraja, TRA, Mtibwa Sugar, Namungo na Mbeya City endapo itafanikiwa kubaki kwenye ligi, lakini sasa limezuka lingine la Polisi Tanzania

Taarifa kutoka vyanzo vya karibu zililiambia Mwanaspoti Polisi Tanzania imeonyesha nia ya kumtaka Matola kutokana na uzoefu wake ndani ya soka la Tanzania pamoja na kazi aliyoifanya akiwa sehemu ya benchi la Simba kwa misimu kadhaa. Kumbuka kuwa Matola aliwahi kuifundisha timu hiyo wakati ilipopanda daraja miaka kadhaa iliyopita na kuipa mafanikio makubwa.

Hata hivyo, licha ya mkataba wa Matola na Simba kufikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu, bado hakuna uamuzi wa mwisho kuhusu mustakabali wake Simba.

“Ni kweli kuna watu wa Polisi wameonyesha kuvutiwa naye kama wakipata nafasi ya kupanda, lakini kwa sasa hakuna jambo lililokamilika. Simba pia bado haijafunga ukurasa kuhusu Matola uongozi nafikiri utakaa naye siku chache zijazo na kufanya mazungumzo kuhusu mkataba mpya, sasa tunapambana kwanza kutafuta ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la CRDB,” kilisema chanzo hicho.

Taarifa zilisema Simba bado kuna tathmini inaendelea juu ya muundo wa benchi la ufundi kwa msimu ujao jambo linaloacha nafasi ya Matola kuendelea kubaki. “Mkataba unaweza kuwa unaelekea mwisho lakini hiyo haimaanishi moja kwa moja ataondoka. Kuna maamuzi ya kiufundi yanayosubiriwa, kwani sio timu moja tu inayomtaka Matola kwa msimu uja.”

Kwa sasa macho yataendelea kuwa kwa pande zote mbili Polisi Tanzania kusubiri hatua yao ya kupanda, huku Simba ikifanya maamuzi ya mwisho kuhusu sura ya benchi la msimu ujao kama itamuacha Matola na kumpandisha John Raphael Bocco au itaendelea naye.