Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matokeo ya mechi za bure Yanga katika CAF

BURE Pict

Muktasari:

  • Katika mechi ya kwanza wikiendi iliyopita Yanga ililala bao 1-0 na leo inahitaji ushindi wa zaidi ya bao mbele ya wapinzani wao ili itinge makundi kwa msimu wa nne mfululizo wa michuano ya CAF.

YANGA jioni ya leo Jumamosi inashuka Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam kurudiana na Silver Strikers ya Malawi katika mechi ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mechi ya kwanza wikiendi iliyopita Yanga ililala bao 1-0 na leo inahitaji ushindi wa zaidi ya bao mbele ya wapinzani wao ili itinge makundi kwa msimu wa nne mfululizo wa michuano ya CAF.

Pambano la leo, mashabiki wameruhusiwa kuingia bure uwanjani ikiwa ni njia ya kutaka kuhamasisha timu ipindue meza na kwenda makundi.

BU 01

Hata hivyo, rekodi zinaonyesha hii sio mara ya kwanza Yanga kuingiza bure mashabiki uwanjani, lakini haijawahi kupata matokeo mazuri mbele ya wapinzani.

Hapa chini ni mechi ambazo kwa uzito wake uliwalazimu mabosi wa Yanga kutoweka kiingilio ili kuhamasisha hamasa ya mashabiki uwanjani, ili kuipa nguvu na wachezaji, ila matokeo hayakuwa mazuri kwa Wananchi.

BU 02

Mei 06, 2007
Yanga 0-0 Esperance (CCM Kirumba)

Juni 08, 2016
Yanga 0-1 TP Mazembe (Kwa Mkapa)

Machi 30, 2024
Yanga 0-0 Mamelodi (Kwa Mkapa)

Hivyo  Yanga leo ina kazi ya kupindua meza kwa kuifunga Silver Strikers, ili kuibariki hii kampeni ya bure kwa mashabiki kinyume na hapo itabidi waifute huo utaratibu kisayansi! 

Nini mtazamo wako, unaamini Yanga leo itapindua meza au...?!

Si Yanga tu, hizi hapa mechi za bure za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika!

Kumekuwa na mjadala mkubwa mitandaoni na mitaani kutokana na pambano la Yanga na Silver Strikers ya Malawi kutokuwa na viingilio.

Hata hivyo,hii mara ya kwanza kwa Yanga kuingiza bure mashabiki au pambano la michuano ya CAF kutokuwa na viingilio.

Hapa chini ni baadhi ya mechi hizo kwa hatua tofauti kwa miaka ya karibuni.


Yanga  vs Mamelodi Sundowns FC 
CAF Champions League
Robo fainali
2023/24

Yanga ilitangaza kuingia bure kwa mashabiki katika 'regular stands' Uwanja wa Mkapa, kampeni ya 'Jaza Mkapa'.


Mamelodi Sundowns FC  vs Espérance de Tunis 
CAF Champions League
Nusu fainali
2023/24
Mashabiki waliovaa jezi ya njano walipewa kuingia bure kama motisha ya kuipa timu nguvu nyumbani.


Al-Hilal Omdurman  vs Al Ahly SC 
CAF Champions League
Robo fainali
2022/23
Klabu iliruhusu mashabiki kuingia bure ili kujaza uwanja wa Al Hilal Stadium na kuongeza morali.


RS Berkane  vs USM Alger 
CAF Confederation Cup
Fainali (mkondo wa kwanza)
2022/23
Serikali ya Morocco ilifadhili tiketi zote kwa mashabiki wa nyumbani kuingia bure kwa wote.


Bibiani Gold Stars  vs JS Kabylie 
CAF Champions League
Raundi ya awali
2024/25
Mashabiki walipewa nafasi ya kuingia bure (viti vya kawaida) isipokuwa VIP pekee waliolipa.


Remo Stars FC  vs US Zilimadjou 
CAF Champions League
Raundi ya awali
2024/25
Mashabiki wa kawaida waliingia bure; ilikuwa njia ya kuvutia uungwaji mkono mkubwa kwa klabu mpya katika michuano hiyo.


Simba SC  vs US Gendarmerie Nationale 
CAF Champions League
Raundi ya awali
2021/22
Simba iliruhusu mashabiki kuingia bure baada ya CAF kuruhusu idadi ndogo ya watazamaji kutokana na katazo la Uviko 19 baada ya awali ilitaka kujaza uwanja.


TP Mazembe 🇨🇩 vs Pyramids FC 
CAF Confederation Cup
Robo fainali
2021/22
TP Mazembe ilitangaza kuingia bure kwa mashabiki wake wa ndani (kutokana na matatizo ya kiuchumi nchini).