Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matokeo ya Azam yamliza Saadun

Muktasari:

  • Azam ilianza kung’olewa katika Ngao ya Jamii kwa kufungwa 4-1 na Yanga katika fainali, kisha ikaaga mapema Ligi ya Mabingwa Afrika ilipochapwa 2-1 na APR ya Rwanda katika mechi za raundi ya kwanza, kabla ya kutolewa Kombe la Shirikisho (FA) na Mbeya City kwa penalti 4-2, na juzi ikishiriki Kombe la Muungano ilitolewa hatua ya nusu fainali kwa kufungwa 2-1 na JKU huko Gombani, Pemba.

KIUNGO mshambuliaji wa Azam, Nassor Saadun amekiri licha ya ubora wake binafsi, lakini kama timu wameshindwa kufikia malengo waliyojiwekea msimu huu na kuondolewa mapema katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu na hata katika michuano mingine waliyoishiriki.

Azam ilianza kung’olewa katika Ngao ya Jamii kwa kufungwa 4-1 na Yanga katika fainali, kisha ikaaga mapema Ligi ya Mabingwa Afrika ilipochapwa 2-1 na APR ya Rwanda katika mechi za raundi ya kwanza, kabla ya kutolewa Kombe la Shirikisho (FA) na Mbeya City kwa penalti 4-2, na juzi ikishiriki Kombe la Muungano ilitolewa hatua ya nusu fainali kwa kufungwa 2-1 na JKU huko Gombani, Pemba.

Kwa sasa timu hiyo imesalia kupambana ili kumaliza katika nafasi ya tatu ya Ligi Kuu Bara na kukata kufuzu ushiriki wa Kombe la Shirikisho Afrika kwa msimu ujao.

Akizungumza na Mwanaspoti, Saadun alisema wameangusha mataji yote waliyokuwa wanayapambania msimu huu kilichobaki ni kuhakikisha timu hiyo inamaliza katika nafasi ya tatu ya ligi.

“Tumeshindwa kuendana na kasi hasa duru la lala salama licha ya kuanza vizuri mzunguko wa kwanza. Nafikiri kila kitu sasa kimepita, tunapambania nafasi ya tatu tutajipanga kwa msimu ujao,” alisema Saadun aliyefunga mabao sita na asisti moja hadi sasa katika Ligi Kuu.

“Tunafanya kila kitu ili tuweze kuwa bora na kuipambania timu yetu, lakini mambo yanakuwa magumu na tunajikuta hatutimizi malengo, inaumiza lakini ndio matokeo, tutajiuliza tunakosea wapi msimu ujao,” aliongeza Saadun aliyetua Azam msimu huu akitokea Geita Gold.

Akizungumzia ligi kwa ujumla, alisema ni ngumu na bora zaidi kwani timu nyingi zimefanya usajili bora na kuongeza changamoto ya ushindani.

“Ilikuwa presha kubwa mimi kujiunga na Azam, mengi yalizungumzwa sikuyapa nafasi, niliwekeza nguvu kuhakikisha nakuwa sehemu ya mafanikio ya timu yangu. Namshukuru Mungu nimeweza kuwa bora nimefunga mabao sita, sio machache licha ya kushindwa kufikia mafanikio ya klabu,” alisema Saadun na kuongeza;

“Ligi yetu inakuwa bora kila msimu tumekwama sasa tumejifunza hatutarajii mteremko msimu ujao.”