Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa 14 Simba, Yanga wakalia kuti kavu

Muktasari:

Mastaa sita wa Simba wako katika wakati mgumu na huenda timu hiyo ikafanya usajili wa majembe yasiyozidi matatu ili kuongeza nguvu katika kutetea ubingwa wa ligi na kufanya vizuri michuano ya Kimataifa.

DIRISHA dogo la usajili linatarajiwa kufunguliwa mwezi ujao ambapo mara nyingi Shirikisho la Soka nchini (TFF) hufungua dirisha hilo Novemba 15 na kufungwa Disemba 15. Usajili huo unatoa fursa kwa timu kufanya marekebisho madogo kwenye vikosi vyao baada ya matokeo ya mechi walizocheza za ligi kuu.
Simba na Yanga tayari wameonesha kuanza mchakato wa usajili kimya kimya ili kujiimarisha zaidi mzunguko wa pili wa ligi ambapo Simba ina kazi mbili kutetea ubingwa na kushiriki michuano ya Mabingwa wa Afrika itakayoanza mwishoni mwa mwezi ujao.
Mwanzoni mwa msimu Simba ilisajili nyota nane ambao ni Meddie Kagere, Cletus Chama, Pascal Wawa, Adam Salamba, Marcel Kaheza, Mohammed Rashid 'MO Rashid', Hassan Dilunga, Abdul Seleman na Deogratios Munishi 'Dida'.
Katika wachezaji hao saba ambao waliwasajili mwanzo wa msimu na Simba wanne ndio wameingia moja kwa moja kikosi cha kwanza ambao ni Dilunga, Chama, Kagere na Wawa wakati Salamba na Kaheza wamekuwa wakitokea benchi wakati Mo Rashid hajacheza mechi hata moja.
Wakati hayo yakiendelea ndani ya kikosi cha mabingwa hao nyota sita huenda wakajikuta katika wakati mgumu kwani ni kama wamekalia kuti kavu kutokana nafasi zao kucheza kuwa finyu.
Nyota hao ni Yusuph Mlipili ambaye alikuwa kikosi cha kwanza msimu uliopita lakini tangu kuanza kwa msimu huu amekuwa na wakati mgumu kwani hajacheza hata mechi moja sawa na MO Rashid.
Nyota wengine ambao kama wamekalia kuti kavu ni Mghana Nicholas Gyan ambaye licha ya kupata nafasi ameshindwa kuonesha kiwango bora huku Said Mohammed 'Nduda', Emmanuel Mseja na Abdul Selemani wakiwa miongoni mwao. 
Mastaa hao sita wa Simba wakiwa katika wakati mgumu huenda Simba akifanya usajili wa majembe yasiyozidi matatu ili kuongeza nguvu katika kutetea ubingwa wa ligi na kufanya vizuri michuano ya Kimataifa.
Miongoni mwa nyota baadhi yao wanaweza kusajiliwa na Simba ni Ibrahim Ajibu ambaye faili lake lipo mezani mwa mabingwa hao, wengine ni Salum Kimenya, Francis Kahata kutoka Gor Mahia na Obrey Chirwa ambao msimu uliopita walikuwa miongoni mwa nyota waliotajwa sana kutua Simba.
Ajibu ambaye anakipiga Yanga mkataba wake unaelekea ukingoni na hajaongeza mkataba mpya, Kimenya wa Prisons yeye yupo tayari kung'oka muda wowote ili mradi tu dau analolihitaji ambapo awali alidai ili asajiliwa na timu yoyote ni lazima apewe Sh 50 milioni ya usajili, Chirwa yeye ambaye msimu uliopita alifanya mauzngumzo za awali na Simba kwasasa yupo huru baada ya kuvunja mkataba na timu yake huko Misri huku Kahata ni lazima  Simba kama watamuhitaji wafanye umafia mkubwa kwa kuvunja mkataba wake na Gor Mahia.
Kocha wa Simba, Patrick Aussems alizungumzia usajili wake kwamba "Akili yangu ilikuwa ni kupata ushindi kwanza katima mechi za ligi lakini lakini itakaposimama nitawapatia viongozi majina au anaina ya wachezaji ambao nitakuwa nawataka lazini hawatazidi watatu na nitaangalia kwanza wale wazoefu katika mechi za Kimataifa na ligi,"
Upande wa Yanga wao mwanzo wa msimu walisajili wachezaji watano ambao ni Deus Kaseke, Mrisho Ngassa, Faisal Salum 'Fei Toto', Heritier Makambo na Nkinzi Kindoki na kumpandisha Poul Godfrey 'Boxer'.
Nyota hao wanne wapya wa Yanga msimu huu watatu waliingia katika kikosi cha kwanza ambao ni Kaseke, Ngassa na Makambo wakati, Kindoki alipata nafasi ya kucheza katika mechi za mwanzo wa ligi na alifanya makosa ambayo yamefanya kumuweka benchi mpaka sasa.
Yanga wakiendelea kutoa dozi mastaa nane wa kikosi hiko huenda wakawa wamekalia kuti kavu kutokana na nafasi finyu za kucheza na dirisha dogo huenda wakaachwa na timu hiyo ambao ni Yohana Mkomola, Baruani Akilimali, Pato Ngonyani, Emmanuel Martin, Mwinyi Haji na Said Mussa.
Wengine Amiss Tambwe na Thabani Kamusoko licha ya kuwa wanapata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kocha Mwinyi Zahera lakini wameshindwa kuwa katika viwango bora pengine kutokana na majeraha ambayo yalikuwa yakiwasumbua.
Mastaa hao nane wa Yanga ambao hueanda wakaachana na timu hiyo katika dirisha dogo wanaungana na wale sita wa Simba kufikia 14 ambao kutoka timu hizo kongwe wamekalia kuti kavu.
Yanga wameingia sokoni kusaka nyota watano ambao watakwenda kuziba nafasi zao na wanaotajwa ni Salumu Kihimbwa kutokea Mtibwa Sugar, Eliud Ambokile (Mbeya City), Meddie Kagere (Simba) na Abdul Rwatubyaye kutokea Rayon Sports ya nchini Rwanda.
Yanga kama watafanikiwa kuwanasa wachezaji hao wataongeza nguvu katika kikosi chao hasa katika mbio za kuwania ubingwa na kufanya vizuri katika mashindano mengine.

Kocha wa Yanga, Zahera alisema "Kwa sasa nimepewa nafasi ya kusajili popote ninapotaka na nimepewa kipaumbele zaidi ya kutoa maamuzi ya mchezaji gani namtaka hivyo nipo mbioni kuleta baadhi ya nyota kutoka katika mataifa matatu ambayo ni Congo, Ghana na Gabon.
"Tayari viongozi nimewatajia majina ya nyota hao na wameanza mazungumzo nao ninaamini watafanya kama nilivyowaagiza kuhakikisha dirisha dogo wananiletea nyota hao ili waongeze nguvu katika kikosi changu ambacho bado kipo katika wakati mgumu mbali na kupata matokeo mazuri katika kila mchezo wanaocheza.
"Pia nataka wachezaji wenye kuzingatia nidhamu nje na ndani ya timu, wanaojuwa thamani ya jezi ya Yanga na wenye viwango vya hali ya juu,"

MSIKIE DR MSOLA
Mtaalamu wa ufundi nchini, kocha Mshindo Msolla anasema kwamba upande wa Simba ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu hawana sababu ya kufanya usajili katika dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa mwezi ujao akitaja sababu zake kwamba;
"Simba wana kikosi kipana, wachezaji wapo wengi wazuri na hawapati nafasi ya kucheza kama Adam Salamba, Marcel Kaheza na Mohamed Rashid, yaani wameenea kila idara kwani hata wachezaji wao wa akiba wana uwezo mkubwa.
"Binafsi ningekuwa kocha wa Simba nisingekuwa na mawazo ya kufanya usajili wakati wa dirisha dogo wlaiopo wangenitosha kabisa kutetea ubingwa na kufanya vizuri mashindao ya kimataifa. Hapo ni kocha mwenyewe jinsi ya kuwatumia.
"Wenye matatizo makubwa ya kikosi ni Yanga ambao wanalazimika kusajili winga wa kulia asilia kwani Mrisho Ngassa muda umeenda, wasajili washambuliaji wawili viongozi kwani Herritier  Makambo anapaswa kuwa mshambuliaji wa pili hawezi kuwa straika kiongozi.
"Zahera anapaswa kusjaili viongo wawili wachezeshaji wa maana kwani Papy Tshishimbi na Thaban Kamusoko hawakidhi haja ya timu kwasasa huku wkaiongeza walinzi wawili au mmoja kutokana na majeraha zinazowaandama," alisema Dr Msolla.

Imeandikwa na Thobias Sebastian, Thomas Ng'itu, Charity James, Charles Abel na Mwanahiba Richar