Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashujaa, Kagera zamfuatilia Kabunda

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo alisajiliwa Namungo msimu nwa 2022/23 akitokea KMC na alishawahi kucheza Mwadui FC ya Shinyanga.

KLABU ya Mashujaa na Kagera Sugar iliyoshuka daraja rasmi zimeanza kumfuatilia mshambuliaji wa Namungo, Hassan Kabunda.

Mshambuliaji huyo alisajiliwa Namungo msimu nwa 2022/23 akitokea KMC na alishawahi kucheza Mwadui FC ya Shinyanga.

Taarifa ilizopata Mwanaspoti ni kuwa Kabunda amemaliza mkataba wa miaka mitatu na Namungo lakini Mashujaa na Kagera zinamfuatilia kwa ukaribu kupata saini yake.

Alipotafutwa na Mwanaspoti Kabunda alisema ni kweli amemaliza mkataba na Wauaji wa Kusini na bado hajasaini mkataba mpya kuendelea kusalia kikosini.

Aliongeza kuwa mbali na kutosaini mkataba mpya pia kuna ofa kutoka klabu mbalimbali zinazohitaji huduma yake ingawa hakuzitaja majina ya timu hizo.

“Huwezi jua lolote linaweza kutokea naweza kubaki Namungo pia nikaweza kufanya kazi sehemu nyingine itategemeana na ofa nzuri nitakayopata,” alisema Kabunda na kuongeza:

“Ligi ilikuwa ngumu msimu huu nimefunga mabao matatu raundi ya kwanza dhidi ya Kagera na juzi hapa dhidi ya Mashujaa.”