Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashindano ya soka ya U 9 yazinduliwa Dar es Salaam

Muktasari:

Kwa muda mrefu hatukuwa na mashindano ya vijana ya umri huo, hivyo Dar Youth Cup itawapa fursa vijana wa umri huo kuonyesha vipaji vyao.

Dar es Salaam.Mashindano ya soka ya vijana wenye umri chini ya miaka 9, 11 na 13 ya Dar Youth Cup yamezinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam.

Mashindano hayo yatafanyika kwa mara ya kwanza chini ya uratibu wa kampuni ya One Plus Communication na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Mkurugenzi wa ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Oscar Milambo amesema mashindano hayo ni neema katika kujenga msingi katika soka la vijana.

"Kwa muda mrefu hatukuwa na mashindano ya vijana ya umri huo, hivyo Dar Youth Cup itawapa fursa vijana wa umri huo kuonyesha vipaji vyao.

Mratibu wa mashindano hayo, Fina Mango amesema  klabu za soka na timu za shule za msingi 20 zitachuana katika mashindano hayo yatakayofanyika Novemba 2 kwenye viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam.

Mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni za Selcom, Vodacom na Toyota yatafanyika kila mwaka mara mbili.

Katika droo ya mechi hizo iliyofanyika leo, timu ya DIS itacheza na Gymkhana, Sunrise International School itacheza na Jakaya Kikwete Youth park, Osterbay primari itacheza na IST, Aghakhan itacheza na shule ya Capston Cristian kwa vijana wa umri chini ya miaka 9.

Kwenye umri wa miaka 11, Karume youth itacheza na Golden Kids, IST na Jakaya Kikwete Youth Center na BBV itacheza na No Escape ya Kigamboni.

Wakati kwa vijana wa umri wa miaka 13, Karume Youth Center itacheza na Magorofani youth academy, Magnet football club itacheza na Mbagara Youth Academy, Jakaya Kikwete itacheza na Winners Academy, Tegeta United itacheza na Matosa youth Foundation.