Mashabiki wamkomalia Metacha
MASHABIKI wa timu ya Yanga baada ya mchezo wao dhidi ya Ruvu shooting wameamua kumsubiri nje kipa wao Metacha Mnata kutokana na kitendo chake cha kuwaonyeshea ishara mbaya yambaya baada ya mechi kumalizika.
Metacha baada ya mchezo kumalizika alizozana na baadhi ya wachezaji wenzake na alipokuwa anaenda vyumbani ndio aliwaonyeshea ishara hiyo mashabiki wa Yanga.
Mashabiki hao ambao hawakufurahishwa na kitendo hicho waliamua kulizunguka gari la timu yao wakimshinikiza kumtaka Metacha aliyetibua furaha yao ya kuifunga Ruvu Shooting
''Tunamsubili aje atuambie kwanini anatuonyeshea vidole kama tusipompata hapa tutamfata nyumbani kwake (akitaja anapoishi mchezaji huyo),” alisikika mmoja wa mshabiki hao.
Hata hivyo shabiki mwingine alipingana na mashabiki wenzake kwa kumtetea Metacha kuwa nae ni binadamu ana moyo wanapaswa waelewe kuwa hakufanya makusudi kutokudaka mpira
''Hawa wachezaji nao ni binadamu tunapaswa kuwaelewa tuwatie moyo sio kuwavunja,” alisema shabiki huyo.
Dakika chache baadae Polisi waliamua kuwafukuza mashabiki hao kwa kutumia mbwa na baadae wachezaji wa Yanga walipanda kwenye basi lao na kuondoka.
Yanga katika mchezo huo wameshinda 3-2 mchezo uliokuwa na ushindani wa hali ya juu kwa dakika zote 90.