Mashabiki kiduchu watinga kwa Mkapa

Saturday September 25 2021
kiduchu pic2
By Thobias Sebastian

Muonekano wa mashabiki katika Uwanja wa Benjamin Mkapa si kama vile ambavyo ulitarajiwa katika mechi hii ya Dabi.

Katika uwanja huu kutakuwa na pambano kubwa la watani wa jadi Simba na Yanga ambalo litaanza saa 11:00 jioni na litakuwa na Ngao ya Jamii.

kiduchu pic1

Hadi kufikia saa 9:00 alasiri upande wa Kaskazini ambako wanakaa mashabiki wa Simba kuna eneo kubwa ambalo viti havina watu kama ilivyo upande ule wa Kusini ambapo wanakaa mashabiki wa Yanga.

Mbali ya burudani mbalimbali ambazo zinaendelea katika uwanja huu hata ule muitikio wa mashabiki kuingia bado ni mdogo.

Jambo hilo linaashiria uwanja huu kutokuwa na mashabiki wengi au kujaa kama ilivyo mechi nyingine kabamba hiyo ya soka nchini inapokutana.

Advertisement
Advertisement