Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manula, Samatta kuwakosa Morocco

TAIFA STARS Pict

Muktasari:

  • Morocco alisema hayo mapema leo wakati akitangaza kikosi cha mastaa 24 kitakachoingia kambini leo Jumamosi, huku pia kipa wa Simba, Aishi Manula akitemwa kwa sababu tofauti.

KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Hemed Suleiman ‘Morocco’ amesema kukosekana kwa nahodha Mbwana Samatta kutaliwezesha benchi la ufundi kuwa na mpango mbadala katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Morocco utakaopigwa Machi 26.

Morocco alisema hayo mapema leo wakati akitangaza kikosi cha mastaa 24 kitakachoingia kambini leo Jumamosi, huku pia kipa wa Simba, Aishi Manula akitemwa kwa sababu tofauti.

Kukosekana kwa Samatta ambaye amekuwa kwenye kiwango bora kwa sasa nchini Ugiriki akiwa na PAOK, kocha huyo alisema ni kutokana na majeraha huku akidai hii ni fursa kwa wachezaji wengine kuonyesha ubora wao.

“Kukosa kwa Samatta kama timu inatakiwa tuwe na plan B (mbinu mbadala) kwenye mpira naamini tuna vijana ambao wanaweza kucheza kwa viwango,” alisema.

Manula aliyekuwa katika kikosi kilichofuzu fainali za Chan na Afcon 2025 hajajumuishwa katika kikosi hicho.

Stars itacheza mchezo huo ugenini imejumuisha wachezaji wanaocheza ndani na nje ya nchi wakiwemo kutoka ligi za England, Denmark, Australia, Irak, Uturuki na Morocco.

Miongoni mwa nyota walioitwa ni Simon Msuva (Al-Talaba SC, Irak), Kelvin John (Aalborg BK, Denmark), na Selemani Mwalimu (Wydad Casablanca, Morocco). 

Morocco, alisisitiza maandalizi yatafanyika  makini ili kuhakikisha kuwa timu inakuwa na ubora wa kushindana na Morocco itakayokuwa nyumbani kwani ni moja ya timu bora Afrika na duniani. 

“Tunataka nafasi ya kwenda Kombe la Dunia na hii ni ndoto ya kila mtu. Tumezingatia tuna wachezaji gani kwa kipindi hiki sasa hawa ni wachezaji ambao tumeona wanaweza kutusaidia kwenye mchezo huo,” alisema Morocco ambaye alipoulizwa juu ya nafasi ya mastaa watatu wa Singida BS, Emmanuel Keyekeh (27), Arthur Bada (22) na Damaro Camara (21) kwenye kikosi chake, Morocco alisema; “Kuhusu wachezaji hao siwezi kuzungumza chochote maana sina uhakika juu ya kubadilisha kwao uraia na hizo taarifa nasikia tu mitandaoni na magazetini.”

Kikosi cha Stars kipo hivi: Makipa ni Yakoub Suleiman (JKT Tanzania), Ally Salim (Simba SC) na Hussein Masaranga (Singida BS) 

Mabeki ni Shomari Kapombe (Simba SC), Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Mohamed Hussein (Simba SC), Pascal Msindo (Azam FC), Mirajy Abdallah (Coastal Union) Ibrahim Abdulla (Yanga), Dickson Job (Yanga), Abdulrazack Mohamed (Simba SC), Ibrahim Ame (Mashujaa FC), Haji Mnoga (Salford City, Uingereza).  Viungo ni Novatus Miroshi (Göztepe FC, Uturuki), Mudathir Yahya (Yanga), Yusuph Kagoma (Simba SC), Feisal Salum (Azam FC), huku washambuliaji ni Charles M’Mombwa (Newcastle United Jets, Australia), Kibu Denis (Simba SC), Simon Msuva (Al-Talaba SC, Iraq), Clement Mzize (Yanga), Iddy Selemani (Azam FC), Selemani Mwalimu (Wydad Casablanca, Morocco) na Kelvin John (Aalborg BK, Denmark).