Mane afagia choo cha msikiti

Muktasari:
Mane ambaye analipwa mshahara pauni 90,000 kwa wiki Anfield, alifunga bao la kwanza wakati Liverpool ikishinda 2-1 dhidi ya Leicester ‘Foxes’ kwenye Uwanja wa King Power Jumamosi iliyopita.
London, England. Mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane amezua gumzo baada ya picha zake akiwa anafagia choo cha msikiti kuzagaa saa moja baada ya kufunga bao katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Leicester City.
Mane ambaye analipwa mshahara pauni 90,000 kwa wiki Anfield, alifunga bao la kwanza wakati Liverpool ikishinda 2-1 dhidi ya Leicester ‘Foxes’ kwenye Uwanja wa King Power Jumamosi iliyopita.
Hata hivyo, picha yake iliyosambaa akisafisha choo katika msikiti imeteka mjadala wa mitando ya kijamii katika picha hiyo ya Twitter ilipata 9,000 retweets na like 18,000.
Picha hiyo ya video ilimuonyesha Mane akijaza ndoo ya maji huku kijana mmoja moja akimsaidia kusafisha sakafu ya choo hicho.
Kwa mujibu ya watu waliotazama picha hiyo kwenye mitandao ya kijamii wanasema picha hiyo ilipigwa katika msikiti wa Al-Rahma uliopo Liverpool.
Mane ni muunimi kiislamu mara zote amekuwa akishangilia mabao yake kwa kusujuod akigusisha kichwa chake chini.
Nyota huyo mwenye miaka 26, amekulia katika kijiji kidogo cha Bambali, kusini mwa Senegal, ambako baba yake ni imam wa msikiti.