Mandonga aamsha shangwe Yanga

Saturday August 06 2022
mandonga pic
By Olipa Assa

BONDIA Karimu Mandonga amezua shangwe baada ya kufika Uwanja wa Benjamin Mkapa, kuisapoti Yanga kwenye tamasha la Wiki ya Mwananchi.

Baada ya Mandonga kufika jukwaa la VIP A la mashabiki wa Yanga, mashabiki walisimama na kuanza kumshangilia.

Baadhi ya mashabiki waliomba kupiga naye picha, huku wakifurahia uwepo wake.


RUBBY APIGA SHOO YA MAANA

Ruby apigaa shoo ya mwaka
MSANII wa bongo fleva, Rubby amefanya shoo ambayo alikuwa anaitikiwa na uwanja mzima, huku mashabiki wakionyesha kufurahishwa naye.

Rubby alianza kuimba nyimbo ya Kingereza ya taratibu, kisha akafuata ya  Kuna Muda ambayo alifanya mashabiki waibue shangwe na kuitikia alichokuwa anaimba.
Kupanda kwa Rubby jukwaani kumeonekana kuwafurahisha na hakuwaangusha kutokana na kujaliwa sauti ya kuvutia.

Advertisement
Advertisement