Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makamu Rais SMZ akunwa  mbio za Yas Z'bar International

RIADHA Pict

Muktasari:

  • Hivyo tuna kila sababu ya kujivunia mbio hizi na kuhakikisha zinakuwa chachu ya maendeleo ya Zanzibar,” amesema Abdulla.

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amepongeza maandalizi na mafanikio ya mbio za Yas Zanzibar International Marathon zilizofanyika leo visiwani Zanzibar kwa mafanikio makubwa.

Abdulla ametoa pongezi hizo wakati wa kilele cha msimu wa tano wa mbio hizo zinazoendelea kuimarisha nafasi ya Zanzibar kama kitovu cha utalii kupitia michezo na kuchochea afya na uchumi wa wananchi.

“Niwapongeze sana kwa maandalizi mazuri waandaaji wa mbio hizi pamoja na taasisi zote zilizoshiriki kuhakikisha Yas Zanzibar International Marathoni inafana. Kama mnavyofahamu, mbio hizi zimekuwa ni jukwaa muhimu katika kuimarisha afya, kuchochea Utalii, kukuza uchumi na kuitangaza Zanzibar kimataifa. Hivyo tuna kila sababu ya kujivunia mbio hizi na kuhakikisha zinakuwa chachu ya maendeleo ya Zanzibar,” amesema Abdulla.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Riziki Pembe Juma amesema Yas Zanzibar International Marathon imesaidia kwa kiasi kikubwa kuchochea ari ya michezo na kukuza Utalii visiwani na kubainisha, mbio hizo ni jukwaa muhimu kwa wanariadha kutoka sehemu mbalimbali kuonyesha vipaji na kutambulika kimataifa kwani mbio hizo zimesajiliwa na Shirikisho la Riadha duniani (World Athletic).

Kwa mwaka huu, mbio hizo zimevutia washiriki kutoka mataifa mbalimbali  kutoka Zanzibar, Tanzania Bara, Kenya, Sudan Kusini, Uganda, Uingereza, Ufaransa, Afrika Kusini, Marekani, Italia, India, China na Japan, huku maelfu ya wananchi wakijitokeza kushiriki katika mbio hizo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mixx,  Angelica Pesha amesema mbio hizo zenye kauli mbiu ya ‘Kila hatua ni Spesho’ kwa mwaka huu wa 2025, zimeendelea zaidi ya ushindani wa riadha. 

“Msimu huu wa tano umeonyesha thamani ya kauli mbiu yetu ya Kila Hatua ni Spesho. Kila mshiriki amekuwa sehemu ya hadithi ya mafanikio ya Zanzibar, kutoka kwa mkazi wa Pemba aliyekimbia kwa mara ya kwanza, vijana kwa wazee waliothibitisha umri si kikwazo,” amesema.

Aliongeza, kwa kipindi cha mwaka mmoja pekee tangu kubadilika kwa chapa, Yas na Mixx zimeona mafanikio makubwa kupitia ushirikiao na Serikali ya Zanzibar.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Hassan Bondi, alimshukuru Rais Mwinyi kwa kushirika katika mbio hizo na vilevile aliwapongeza washindi na kuwashukuru washirika wengine.

"Tunawashukuru sana washirika wetu na wakimbiaji wote kwa kuungana nasi katika juhudi za kuchochea Utalii, Michezo, Afya na Biashara hapa Zanzibar," amesema Bondi.

Katika mbio hizo ilishuhuhudiwa Mkenya Catherine Syokau akishinda mbio za kilomita 21 kwa wanawake, huku Mtanzania Maohhando Ako akishinda kwa wanaume, ilihali katika km 10 nafasi zote za kwanza kwa wanaume na wanawake zilichukuliwa na Watanzania.

Mwanadada Sisila Ginoka alishinda kwa upande wa wanawake na Mathias Sylvester alikuwa mbabe wa mbio hizo kwa wanaume.