Makambo, Djuma waongoza jeshi la Yanga

Muktasari:

  • Yanga inakaa kambi ya wiki mbili nchini Moroccco kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi.

WACHEZAJI wapya wa Yanga, Heritier Makambo na Djuma Shaban ni miongoni mwa nyota waliopo katika kikosi kinachokwenda nchini Moroccco kwa ajili ya kambi ya wiki mbili.

Wachezaji wa Yanga waliingia katika uwanja wa ndege Julius Nyerere Terminal 3 saa 6:30 mchana na moja kwa moja waliingia ndani bila kuwa na mazungumzo yoyote.

Safari ya Yanga kwenda Morocco || Djuma, Makambo waongoza msafara

Nyota hao wa Yanga walikuwa wamevalia sare walikuwa wanaongozana huku wakiwa hawana maneno zaidi ya kufata maelekezo.

Meneja wa klabu hiyo, Hafidh Saleh ndio alikuwa anaongoza msafara wa wachezaji hao pia hata upande wa ndani alikuwa anatoa maelekezo namna ya kufanya na wachezaji hao walikuwa wanafaya kila kinachoelekezwa.

Wachezaji wengine waliopo katika msafara huo ni Fiston Mayele, Yassin Mustapha, Kibwana Shomari, Deus Kaseke, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Ramadhan Kabwili, Tonombe Mukoko, Adeyum Saleh na Farid Mussa.

Wengine ni Abdallah Shaibu, Paul Godfrey, Dickson Ambundo, Zawad Mauya, Yusuph Athuman, Mapinduzi Balama, David Bryson, Jesus Moloko, Feisal Salum Ditram Nchimbi na Eric Johola.