Majaliwa kuwashuhudia Stars

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ndiye atakuwa mgeni rasmi wa mechi ya kirafiki ya kimataifa, ambapo Taifa Stars kesho Jumapili Oktoba 11, 2020 itaikaribisha Burundi, Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi amethibitisha Majaliwa kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo ambao Stars, itakabiliana na Burundi.

Amesema mechi hiyo, imepangwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia (FIFA), itawahusisha wachezaji wa Stars wanaocheza ndani na nje,watakaoongozwa na nahodha Mbwana Samatta.

"Kwasababu hiyo, tunawasisitiza Watanzania,kujitokeza uwanjani Jumapili saa 10:00 jioni kwa wingi kuishangilia timu yetu,ambayo itatumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mechi nyingine za kimataifa za kimashindano zitakazoanza Novemba mwaka huu," amesema  Abbasi na ameongeza kuwa.


"Wanachi watumie kadi maalum za kuingia uwanjani za N-Card kukata tiketi zao mapema, kuhusu viongozi wa serikalini, siasa, asasi za kijamii na sekta binafsi wanaotaka kukaa eneo la VVIP na kuingia maeneo mengine, wawasiliane na meneja wa uwanja kwa ajili ya utaratibu mahsusi,"amesema.