Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Machupa: Simba hii ndio bora zaidi

Muktasari:

Machupa ambaye kwa sasa amehamishia makazi yake nchini Sweden, baada ya kustaafu saoka la ushindani akijikita kwenye masuala ua kifundi.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Athuman Machupa, amemmumuisha kiungo Haruna Moshi ‘Boban’ kwenye kikosi cha bora cha Wekundu wa Msimbazi.
Machupa, ambaye sasa amestaafu soka la ushindani, amesema kuwa kati ya mwaka 1999 hadi 2007 Simba ilisuka kikosi tishio kwenye Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati hivyo, kuzinyima raha timu pinzani.
Kwenye kikosi hicho, Machupa alikuwa miongoni mwa nyota wanaosumbua kwenye safu ya ushambuliaji akisaidia kuwabeba Wekundu hao kunasa matokeo bora uwanjani.


KIKOSI CHAKE HIKI
Machupa anasema kuwa kwenye kikosi chake ambacho anaamini ndio bora zaidi wakati akikipiga klabuni hapo, golini anasimama Mohammed Mwameja akisaidiwa na Juma Kaseja, ambaye alikuwa sub.
"Juma (Kaseja) tumepata mafanikio mengi tukiwa pamoja Simba ikiwemo kuifunga Zamalek na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara bila kupoteza mchezo, lakini bado Mwameja alikuwa moto. Wakati ule langoni mwa Simba kinaingia chuma kinatoka chuma," alisema Machupa.
Nyota wengine ambao wanaunda kikosi chake kuanzia eneo la ulinzi hadi washambuliaji kuna, Said Swedi, Ramadhan Waso, Victor Costa, George Masatu, Seleman Matola, Ulimboka Mwakingwe na Rajabu Msoma (sasa ni marehemu).
Pale jirani ya lango la adui ambao wana jukumu la kupasia nyavuni, anasimama mwenyewe kwenye namba tisa akicheza sambamba na Shaban Kisiga (namba 10) na Boban anasimama namba 11.
"Hicho ndicho kikosi bora cha Simba ambacho kilitamba sana enzi nikicheza Msimbazi," alisema Machupa jana katika mahojiano maalum ambayo yatachapishwa hivi karibuni.
Mshambuliaji huyo ameizungumzia tofauti ya Simba enzi akicheza kwenye timu hiyo na sasa, akisema kuna tofauti kubwa.
"Mabadiliko yapo mengi sasa kuanzia mfumo wa uendeshaji wa klabu na vitu vingi tu, Simba ya sasa ina uwanja wake wa mazoezi, sisi tulikuwa tunahangaika ni wapi tukafanyie mazoezi.
"Wachezaji wanalipwa vizuri, tofauti na wakati wetu kuna kipindi hata mishahara kupata ilikuwa tabu, lakini sasa mambo yamebadilika na ndio mpira wa kisasa unavyotaka.
Machupa, ambaye tangu mwaka 2009 anaishi nchini Sweden, pia amefunguka kuhusu idadi ya nyota wa kigeni na kushauri kwamba, inaweza kuongezeka maradufu.
"Hata wakifika 20 ni sawa, lakini wachezaji hao wawe na uwezo mkubwa kushinda na wazawa ili tujifunze kupitia wao, lakini sio wachezaji wa kigeni wanakuja kukaa benchi,".