Ligi ya Kikapu Dar mambo ni moto

Muktasari:
- Kwa sasa ligi hiyo imesimama ili kutoa nafasi ya kujiandaa kwa timu za mikoa zinazokwenda kushiriki michuano ya Taifa Cup, kuanzia Juni 24 hadi Julai 4, baada ya hapo itaendelea tena.
MECHI saba za mwisho kabla Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam ( BDL) kusimama kupisha michuano ya Taifa Cup, timu zilionyesha ushindani mkali uliyowapa mashabiki burudani katika viwanja vya Don Bosco vilivyopo Upanga, Dar es Salaam.
Kwa sasa ligi hiyo imesimama ili kutoa nafasi ya kujiandaa kwa timu za mikoa zinazokwenda kushiriki michuano ya Taifa Cup, kuanzia Juni 24 hadi Julai 4, baada ya hapo itaendelea tena.
Baadhi ya mechi zilizokuwa tafu ni Mgulani Stars 41-53 Twalipo, Jeshi Stars 67-59 Vijana QueensJKT 56-44 Vijana na UDSM Outsiders 56-66 Pazi ambapo wachezaji walikuwa wanalazimika kufunga vikapu nje ya 18 ili kupata pointi, wachezaji walitumia nguvu na kukabana mtu na mtu.
Mechi kama Dar City iliyoshinda vikapu 103 kwa 57 dhidi ya Chui, wachezaji wa timu hiyo walionyesha kiwango kikubwa zaidi, kuliko wapinzani wao ndiyo maana ilipata ushindi mnono.
Mashabiki walijaa katika viwanja hivyo kupata burudani na kuzisapoti timu zao, zilizofanikiwa kuibuka na ushindi kila mchezaji na benchi la ufundi walipata Shilingi 87,500 baada ya mechi, jambo linaloongeza ushindani zaidi.
Matokeo ya jana BD
Mgulani Stars 41-53 Twalipo Queens
Tausi Royals 80-26 Kigamboni Queens
JKT Stars 74-54 Polisi Stars
Dar City 103-57 Chui
Jeshi Stars 67-59 Vijana Queens
JKT 56-44 Vijana
UDSM Outsiders 56-66 Pazi