Kwa Chilunda ni uamuzi mgumu

DILI la mshambuliaji wa Simba, Shaban Chilunda kujiunga na klabu ya KMC nusra liingie mchanga, kisa kilikuwa ni mambo ya maslahi.

Nyuma ya kutua kwake KMC, yapo mambo ambayo viongozi wa Simba wameyafanya kuhakikisha mchezaji huyo hakosi timu.
Simba ilikaa mezani na viongozi wa KMC, ili kusaidiana kulipa mshahara wa mchezaji huyo, ombi hilo halikukubalika kwani ilionekana hakuwa kwenye mahitaji yao.

Jambo la kwanza Simba ilikuwa inataka Chilunda apate nafasi, lilipoonekana hilo lina mwelekeo,basi ikaamua kukaa kando na mchezaji huyo, ili kujua jinsi ya kumlipa.

Licha ya  Chilunda kukubaliwa na KMC, mshambuliaji huyo kwenye mfumo wa TMS usiku huu tayari imeonekana kuombwa na timu nyingine hivyo KMC inapambana kumuingiza kwenye mfumo.

Simba pekee ndio yenye uwezo wa kuamua hatma ya mchezajihuyo usiku huu kwa kukataa maombi ya timu zingine kwenye mfumo kabla ya dirisha halijafungwa.

Chilunda amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili na ameitumikia timu hiyo kwa miezi sita.