Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumekucha, Lilepo ajiondoa Al Hilal

Muktasari:

  • Lilepo unavyosoma gazeti hili yuko kwao DR Congo jijini Kinshasa huku taarifa za kutakiwa na Yanga zikiendelea kuvuma kwa kasi huku klabu yake ikiwa nchini Morocco.

WAKATI Yanga ikivumishwa kumhitaji mshambuliaji wa Al Hilal, Makabi Lilepo mwenyewe ameshtua baada ya kujiondoa kwenye kambi ya timu hiyo akishinikiza kutaka kuondoka klabuni hapo.

Lilepo unavyosoma gazeti hili yuko kwao DR Congo jijini Kinshasa huku taarifa za kutakiwa na Yanga zikiendelea kuvuma kwa kasi huku klabu yake ikiwa nchini Morocco.

Al Hilal imechagua kucheza mechi zake za Ligi ya Mabingwa nchini Morocco ikikutana na mteremko wa kutinga hatua ya kwanza ya mtoano baada ya wapinzani wao Wau Salaam ya Sudan Kusini kujiondoa kwenye mashindano hayo.

Kabla ya uamuzi huo tayari Lilepo alikuwa ameshatimka kwenye kikosi hicho akirudi kwao Kinshasa huku mmoja wa mabosi wa klabu hiyo akiliambia Mwanaspoti kuwa mshambuliaji huyo anashinikiza uongozi kumuacha huru aondoke zake.

Kwenye barua ya Lilepo ametaja kuwa sababu kubwa inayomfanya kuchukua uamuzi huo ni ligi ya nchini humo kutoendelea mpaka sasa akidai hatua hiyo inampotezea kipaji chake.

“Klabu yetu bado haijajibu barua yake lakini hapa kwenye kambi alishaondoka muda unakaribia wiki sasa nasikia yuko Congo akiendeleza huo mgomo,” alisema bosi wa Al Hilal na kuongeza;.

“Ni kweli tumekutana na hiyo changamoto ya wachezaji wetu wengi bora kutaka kuondoka baada ya hali ya kule Sudan kutokaa sawa, wapo wengine wametumia hii hali kama fursa ya kuhamia timu nyingine.”

Yanga inasaka mshambuliaji wa kati atakayekuja kuboresha safu yao ya ushambuliaji huku Lilepo akiwa mmoja wa mastaa ambao wanatajwa kusakwa na mabosi wa mabingwa hao wa Tanzania.

Mapema Mwanaspoti linafahamu kuwa Yanga ilikuwa na hesabu za kumsajili Lilepo ambapo wawili hao walikuwa wanashindana kwenye mshahara pekee Mkongomani huyo akitaka alipwe dola 14,000 kwa mwezi.

Mbali na Lilepo pia Yanga inahusishwa kuwapigia hesabu washambuliaji wengine wawili wazawa George Mpole na Simon Msuva endapo watakosa muafaka wa kumchukua mshambuliaji wa kigeni.

Hata hivyo, Yanga kama itakubaliana na Lilepo mtihani mkubwa utabaki nani akatwe katika orodha ya wachezaji wao wa kigeni 12 ambao wanao sasa kwenye timu yao ikiwa tayari wameshakamilisha idadi kamili ya kikanuni.