Kumbe Lukaku kakimbia bifu kali

Muktasari:
Imeelezwa kwamba mchezaji huyo alifahamu wazi kuwa suala lake la kupata namba au kukaa kwa amani katika klabu hiyo lisingewezekana tena
LONDON, ENGLAND.Imefahamika kuwa kisa cha nyota wa Manchester United Romelu Lukaku kuondoka katika klabu ya hiyo ni ugomvi baina yake na kocha msaidizi Mike Phelan.
Imeelezwa kwamba mchezaji huyo alifahamu wazi kuwa suala lake la kupata namba au kukaa kwa amani katika klabu hiyo lisingewezekana tena. Ndio maana akaamua kuondoka zake. Taarifa kutoka ndani ya klabu zinasema kuwa ugomvi wao ulikuwa mkubwa wakati wa mechi za kujiandaa na msimu huko Mashariki ya Mbali.
Imeelezwa kwamba wakiwa Shanghai, wachezaji walitakiwa kujipanga katika ghorofa ya tatu ya hoteli kwa ajili ya kuona kama wote wapo, tayari kwa kwenda uwanjani kukwaana na Spurs. Lukaku hakuwepo, walinzi wakamwabia kocha Ole Solskjaer na kabla hajajibu kitu, kocha msaidizi alidakia na kusema gari liondoke bila ya mchezaji huyo.
Ilibidi Lukaku atafute usafiri kwenda uwanjani. Kitu hicho kilimuudhi Lukaku lakini Phelan alimwambia kuwa hilo ni onyo lake.