Kocha Prisons hali tete, aiwaza Coastal

Muktasari:

  • Ally ambaye alitua kikosini humo mwishoni mwa mwezi Oktoba akichukua nafasi ya mtangulizi wake, Fred Fe-lix ‘Minziro’ aliyesitishiwa mkataba kutokana na matokeo mabovu.

Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Ahmad Ally ameanza kuonja joto la jiwe kufuatia matokeo yasiyoridhisha anayoendelea kupata na kumuweka katika wakati mgumu.

Ally ambaye alitua kikosini humo mwishoni mwa mwezi Oktoba akichukua nafasi ya mtangulizi wake, Fred Fe-lix ‘Minziro’ aliyesitishiwa mkataba kutokana na matokeo mabovu.

Kocha huyo wa zamani wa KMC, alikuwa na mwanzo mzuri alipoiongoza timu hiyo katika mechi nne za mwanzo na kushinda tatu na sare moja kabla ya kupoteza dhidi ya Yanga 2-1.

Katika mechi sita za hivi karibuni, Prisons imeshinda mchezo mmoja dhidi ya Simba 2-1, ikipoteza mmoja mbele ya Mtibwa Sugar 2-1 na kufululiza sare na kushuka hadi nafasi ya sita kwa pointi 31.

Maafande hao wanatarajia kuwa kibaruani tena leo dhidi ya Coastal Union walio nafasi ya nne kwa alama 32, mechi ikipigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Akizungumzia matokeo hayo, kocha huyo zao la kocha wa zamani wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Sylivester Marsh, alikiri kutokuwa mazuri huku akijipa matumaini kuwa mambo yatanyooka.

Alisema baada ya kusimama ligi kwa muda, amekuwa na muda mzuri wa kuandaa vijana wake na leo Jumatatu anaamini wanaweza kushinda mechi dhidi ya Wagosi na kufuta gundu la kukosa ushindi kwenye mechi zilizopita.

“Lazima tukubali ligi ni ngumu haswa mechi hizi za lala salama, kila timu imejipanga kufikia malengo, kuna am-bao wanapambania ubingwa, nafasi nne za juu na kukwepa kushuka daraja.

“Kimsingi nimekuwa na muda mzuri na vijana wangu tukisahihisha makosa yaliyoonekana na matarajio yetu ni kureje-sha ari na furaha kuanzia mechi hii na Coastal Union,” alisema kocha huyo.