Kocha mpya wa Yanga atua

Tuesday April 20 2021
kocha mpya pic
By Mwandishi Wetu

KOCHA mpya wa Yanga, Nasreddine Nabi amewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 3.

Kocha huyo aliwasili uwanjani hapo saa 8:45 mchana akiwa na msaidizi wake pamoja na wakala wake Abdul Mussa kutoka kampuni ya Sifeza.

Mwenyeji wao Hersi Said ambaye ni Makamu mwenyekiti wa kamati ya mashindano Yanga, aliwapokea na kusema moja kwa moja ataenda kuonge a zaidi makao makuu ya klabu hiyo.

KOCHA MPYA PIC2

Mwanaspoti lilipomuhoji kocha huyo alisema kwa kifupi kwamba anaifahamu Yanga na anafurahi kuja kufanya nao kazi.

“Nimekuwa nikiifatilia Yanga tangu tumeanza kufanya nao mazungumzo,nina furaha kuwa hapa na naamini nitafanya vizuri.”

Advertisement

Kocha huyo anatarajia kusaini mkataba na timu hiyo na mara moja kuanza kazi akirithi mikoba ya Cedric Kaze aliyetimuliwa.

Advertisement