Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Mingange ajivunia Songea United

SONGEA Pict

Muktasari:

  • Mingange aliyezifundisha Ndanda FC, Mbeya City na Tanzania Prisons, alisema sababu iliyowakwamisha kupanda Ligi Kuu Bara msimu ujao ni kutokana na ushindani mkubwa wa wapinzani wao, kuanzia nguvu ya kiuchumi na wachezaji bora waliokuwa nao.

KOCHA wa Songea United, Meja Mstaafu, Abdul Mingange amesema licha ya kujiunga na timu hiyo kwa kipindi cha miezi sita, ila anajivunia maendeleo yaliyopatikana kwa msimu huu, licha ya kukiri changamoto kubwa kwao ilikuwa ni ugumu wa ratiba.

Mingange aliyezifundisha Ndanda FC, Mbeya City na Tanzania Prisons, alisema sababu iliyowakwamisha kupanda Ligi Kuu Bara msimu ujao ni kutokana na ushindani mkubwa wa wapinzani wao, kuanzia nguvu ya kiuchumi na wachezaji bora waliokuwa nao.

“Kwanza hapa tulipo kiukweli najipongeza kwa sababu viongozi waliniambia lengo ni timu ibaki Championship, ila nikasema tunaweza kupambana zaidi ya hapo, tunashukuru malengo hayo tumefikia na tunajipanga tena msimu ujao,” alisema Mingange.

Kocha huyo aliyejiunga na timu hiyo Desemba 10, 2024, akitokea Stand United kuchukua nafasi ya Ivo Mapunda, alisema aliingia kipindi kigumu kutokana na ratiba ngumu kwa mechi za ugenini, ila anawashukuru wachezaji kwa kupambana.