Kocha KMC tulitarajia ushindi.

Muktasari:
- Kondo amesema kuwa alitarajia ushindi huo kwenye mchezo wa kutokana na kujipanga vyema kuwazuia Azam ambao walijua ubora ao uko sehemu gani.
BAADA ya KMC kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam kwenye mchezo wa jana kocha mkuu wa timu hiyo Habib Kondo ameelezea tathimini yake kwa ujumla juu ya mechi hiyo.
Kondo amesema kuwa alitarajia ushindi huo kwenye mchezo wa kutokana na kujipanga vyema kuwazuia Azam ambao walijua ubora ao uko sehemu gani.
“Tulitegemea kushinda mechi hii kutokana na namna tulivyojiandaa, tunamshukuru mungu tumepata alama tatu ambazo zitatusogeza kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi kuu,” amesema na kuongeza,
“Ushindi huu, utaongeza morali ya wachezaji wetu kuelekea michezo mingine ijjayo ya ligi, pia nimeona wapi tunatakiwa kufanyia kazi zaidi kwa maana ya uchezaji wa timu kwa ujumla ili ushindi huu uwe endelevu,” amesema Kondo.
Ushindi huo unawafanya KMC kufikisha alama 18 na kusogea mpaka nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu baada ya kucheza mechi 11.
..............................................
Na Ramadhan Elias