Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha KMC, Mubesh aona mwanga KMC

Muktasari:

  • Mei 14, mwaka huu ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora, KMC iliichapa Tabora United bao 1-0 lililotokana na penalti ya dakika ya 58 kupitia Deogratius Kulwa ikiwa ni ushindi wa kwanza kwa kocha huyo aliyeziba nafasi iliyoachwa wazi na Kally Ongala.

KOCHA wa KMC, Adam Mbwana Mubesh, amesema ameona mwanga tangu aanze kukinoa kikosi hicho, huku akisema kilichobadilika kwa sasa ni mipango tu na anafurahia ushindi alioupata dhidi ya Tabora United.

Mei 14, mwaka huu ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora, KMC iliichapa Tabora United bao 1-0 lililotokana na penalti ya dakika ya 58 kupitia Deogratius Kulwa ikiwa ni ushindi wa kwanza kwa kocha huyo aliyeziba nafasi iliyoachwa wazi na Kally Ongala.

Mechi hiyo inakuwa ya pili kwa Mubesh tangu akabidhiwe benchi la ufundi la KMC baada ya kupoteza ya kwanza dhidi ya Simba kwa mabao 2-1.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mubesh alisema kwa muda aliohudumu kikosini hapo hawezi kusema kwamba ameibadilisha timu hiyo kwa kiasi kikubwa.

Aliongeza, timu hiyo inahitaji umoja kushinda mechi mbili zilizosalia dhidi ya Mashujaa Juni 18 na Pamba Jiji Juni 22.

“Nimerejea nyumbani lakini hakuna kikubwa nilichokibadili, kwa muda nilioteuliwa sio rahisi kubadili kikosi, hivyo unafuata muongozo wa mtangulizi wako unapita mule mule,” alisema kocha huyo na kuongeza.

“Ninafurahishwa na utimamu wa akili kwa wachezaji inafanya kazi yangu kuwa rahisi na naamini mechi zilizosalia tutapata matokeo mazuri.”

Kocha huyo alichukua mikoba ya Kally Ongala aliyeiongoza katika mechi 15 za Ligi Kuu Bara ambapo kati ya hizo, alishinda nne, sare nne na kupoteza saba.

Ongala aliyeifundisha pia Azam FC akiwa kocha wa mpito na kocha wa washambuliaji, alijiunga na KMC Novemba 14, 2024, akichukua nafasi ya Abdihamid Moallin aliyetimkia Yanga.

Awali, Mubesh aliwahi kufanya kazi Simba kabla ya kujiunga na KMC akiitumikia nafasi ya kocha wa viungo na utimamu wa mwili yaani (Fitness Coach), akiwa na taaluma ya ukocha inayompa fursa kubwa ya kukiongoza kikosi hicho cha Kinondoni.

Kocha huyo alikuwa sehemu pia ya benchi la ufundi la timu ya taifa ya Tanzania ya wavulana chini ya umri wa miaka 15, iliyotwaa ubingwa wa Mashindano ya Mabingwa wa Soka Shule za Afrika 2025, yaani African Schools Football Championship huko Ghana.