Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha JKT atambia beki yake

Kocha wa Yanga, Kosta Papic katika moja ya pozi zake uwanjani. Hatma ya kocha huyo bado haijafahamika na huenda akaikimbia Yanga baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi kuu mwezi April kwa kile kinachodaiwa kuwa hatimiziwi matakwa yake na Yusuf Manji kwa mujibu wa mkataba.

OLIVER ALBERT KOCHA wa JKT Ruvu, Charles Kilinda amesema kurejea kwa mabeki wake wa kati Shaibu Nayopa na George Minja kutaiongezea nguvu timu hiyo kuibana kwenye mechi baina ya timu hizo mbili leo Jumamosi. Wachezaji hao walikosa mechi mbili zilizopita dhidi ya Azam na Moro United kutokana na kuwa na kadi nyekundu walizoonyeshwa wakati wa mechi yao dhidi ya Kagera Sugar. Kilinda alisema kikosi chake kiko vizuri kuizuia kasi ya Simba na kuongeza kuwa watakomaa ili kuibuka na ushindi. "Mechi ni ngumu, lakini nafurahi kuona mabeki wangu wamerejea na hiyo itatuongezea nguvu ya kufanya vizuri katika mechi hii, ingawa nitawakosa Sosthenes Manyasi na Oscar Sagupina, ambao wapo kozi. "Nimewaambia wachezaji wangu wanachotakiwa ni kulinda heshima, hatutaki kuona makosa kama ya mzunguko wa kwanza yanajirudia, ushindi ni muhimu," alisema Kilinda, ambaye timu yake ilichabangwa na Simba 4-1 kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza. JKT katika siku za karibuni imerejesha makali yake na itaingia ikiwa na matumaini katika mchezo kufuatia ushindi wake wa 2-0 iliyoupata dhidi ya Moro United hivi karibuni.