Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KMKM, Mlandege zatinga nusu FA kibabe

KMKM Pict

Muktasari:

  • Bingwa wa msimu uliopita ilikuwa ni Chipukizi ya Pemba iliyopewa ushindi mezani dhidi ya JKU iliyovunja pambano matokeo yakiwa ni 1-1, japo timu hiyo ya Pemba ilishindwa kuiwakilisha nchi katika michuano ya CAF na badala yake ilienda Uhamiaji.

WABABE wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL), KMKM na Mlandege, jioni ya leo Jumatano zimetinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Zanzibar (ZFF Cup) kanda ya Unguj,  baada ya kushinda mechi za robo fainali.

KMKM iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya New King katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mao Zedong, mjini Unguja.

Katika mchezo huo, jumla ya kadi tano za njano zimetolewa kwa kwa wachezaji wa timu hizo  tatu zikienda KMKM na mbili kwa New King.

Bao la kwanza la KMKM lilifungwa na Ilyasa Moh'd dakika ya 36 kabla ya Abrahman Othman kuongeza la pili dakika ya 68  huku Is-haka Said alimalizia udhia dakika ya 72 na kuwahakikishia Mabaharia hao kwenda nusu fainali ya michuano hiyo ambayo bingwa wake uiwakilisha nchi katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Mabao ya kufutia machozi ya New King, yote yaliwekwa kimiani na Mohammed Abdallah katika dakika za 82 na 83.

Katika mechi nyingine ya robo fainali iliyopigwa pia leo  Mlandege ilifanya kwwli kwa kuing'oa Wakati Kikungwi Stars kwa kuichapa kwa penalti 5-4.

Mechi hiyo  ililazimika kuingia katika hatua ya penalti baada ya dakika 90 kumalizika kwa timu hizo kushindwa kufungana.

Bingwa wa msimu uliopita ilikuwa ni Chipukizi ya Pemba iliyopewa ushindi mezani dhidi ya JKU iliyovunja pambano matokeo yakiwa ni 1-1, japo timu hiyo ya Pemba ilishindwa kuiwakilisha nchi katika michuano ya CAF na badala yake ilienda Uhamiaji.

Michuano hiyo kwa robo fainali inaendelea tena leo jioni kwa kanda ya Pemba, Jamhuri itavaana na Chipukizi, huki Elgado itaumana na Super Falcon. Kwa kanda ya Unguja,  Mafunzo itapepetana na Kundemba, wakati Malindi itaonyeshana kazi na Black Sailors. Kwa Pemba mechi zitapigwa Uwanja wa FFU Finya na Unguja zikipigwa viwanja vya Mao.

Pemba zimeshapata timu nne za zitakazochuana nusu fainali ambazo ni watetezi, Chipukizi, Junguni United, Wembe na Super Falcon.