KMC yampigia hesabu Lucas Kikoti
KLABU ya KMC iko kwenye mazungumzo ya kumpata kiungo wa Namungo, Lucas Kikoti ili akaichezee timu hiyo.
Kocha wa KMC, Jamhuri Kihwelo 'Julio' ni pendekezo la mchezaji huyo kwa sababu anataka kuungana naye tena kwani kabla ya hapo walishawahi kufanya kazi pamoja wakati akiifundisha Namungo.
Wakati KMC ikihitaji saini ya Kikoti ila tayari imewasajili, Juma Shemvuni aliyekuwa anaichezea Mbeya City iliyoshuka daraja, Muhsin Malima (Dodoma Jiji) na Rodgers Gabriel aliyetoka Pamba.
Kabla ya kutua Namungo misimu mitatu iliyopita akiipandisha Ligi Kuu, aliwahi kuichezea Majimaji Songea kwa misimu mitatu mfululizo kuanzia 2015-2018.