Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kizazi kipya cha viungo wa kati wanaoitikisa dunia

Muktasari:

Baada ya kuondoka kwa zama hizo, kukaja zama nyingine. Hii tuiite kizazi kipya. Mwanaspoti linakuchambulia, viungo 10 wa kati, wanaotikisa duniani kwa sasa.

Safu ambayo kwa hakika ndiyo inayoamua nini kifanyike uwanjani ni safu ya kiungo wa kati. Hawa watu buana, wanajua mpira.

Ni safu inayotoa mafundi wa mpira. Mafundi hasa. Anzia tu enzi za kina Johan Cruyff, wakaja kina Andrea Pirlo, Ronaldinho hadi enzi za Andres Iniesta na Xavi.

Baada ya kuondoka kwa zama hizo, kukaja zama nyingine. Hii tuiite kizazi kipya. Mwanaspoti linakuchambulia, viungo 10 wa kati, wanaotikisa duniani kwa sasa.

10. Thiago Alcantara

(Bayern Munich)

Majeraha yamekuwa sehemu kubwa ya maisha yake ya soka. Dunia haijamfaidi kikamilifu, lakini licha ya hayo yote, ni viungo wachache tu ndio wanaoukaribia uwezo wa Thiago Alcantara (27).

Kiungo huyu wa Bayern Munich, mwenye damu ya Kibrazil na uzao wa akademi ya La Masia, ni mmoja wa viungo bora wa kati duniani, ambaye miguuni mwake, ana vitu viwili; ukichaa wa soka la mitaa ya Amerika Kusini na ufundi wa soka la Kihispania.

Ni fundi wa kuuchezea mpira na kuumiliki pia. Ana uwezo wa kupenya misitu migumu. Akiwa na mpira mguuni ni ngumu kumpokonya na sifa yake kuu, uwezo wa kufunga mabao.

9. Bernardo Silva

(Man City)

Huu umekuwa mwaka mzuri sana katika maisha ya soka ya Mreno huyu.

Msimu wa 2017/18, Bernardo Silva, alianza kwenye mechi nne tu, kabla ya Krismasi, lakini taratibu akaanza kuteka safu ya kiungo yaMan City.

Hivi sasa, ni mmoja kati ya wachezaji tegemeo katika kikosi cha Pep Guardiola. Ni mmoja wa viungo bora wa kati EPL na duniani. Ana kasi, utundu wa kuuchezea mpira, na uwezo mkubwa wa kufunga na kuanzisha mipango ya kupata mabao.

Silva, aliyesajiliwa kwa Pauni 43 milioni, akitokea Monaco, awali alitumika kama winga, lakini kukosekana kwa Kevin De Bryune, ambaye amekuwa majeruhi kwa muda mrefu, kulimpa nafasi ya kuionesha dunia, uwezo wake mwengine.

8. Paul Pogba (Man United)

Katika utawala wa Jose Mourinho, Pogba alikuwa ni mmoja wa viungo wabovu, kiasi cha kuonekana kuwa kikwazo katika kikosi cha Manchester United. Ujio wa Ole Gunnar Solskjaer, ukaja na mambo mapya. Pogba amebadilika!

Alikuwa analazimishwa kukaba zaidi. Hakuruhusiwa kupanda mbele. Hili lilikuwa tatizo, kwani Pogba ni kiungo mshambuliaji. Anapenda kufunga mabao. Hivi sasa, dunia inafaidi kipaji chake kwa sababu, ana uhuru wa kucheza katika nafasi anayoimudu zaidi.

Kwa sasa anafanana na kiasi cha Pauni 89 milioni, zilizotumika kumng’oa Juventus (2016). Ametoa asisti saba mpaka sasa, anaendesha safu ya kiungo ya United, na kuamua wacheze vipi. Mabao yake tisa, yanathibitisha uwezo wake.

7. Sergio Busquets

(Barcelona)

Ni zaidi ya mwongo mmoja, tangu Sergio Busquets, alipotambulishwa katika ulimwengu wa soka. Katika msimu wake wa kwanza, aliisaidia Barcelona ya Pep Guardiola, kushinda mataji matatu.

Kiungo huyu wa kati, anayetumika sana kwenye ukabaji, kwa sasa ana umri wa miaka 30, na ameichezea Blaugrana zaidi ya mechi 500. Atabaki kuwa mmoja wa viungo bora wa kati (namba sita), ambao dunia imepata kuwashuhudia.

6. Miralem Pjanic (Juve)

Real Madrid, wanahusishwa na wachezaji wengi sana tangu Zinedine Zidane, aliporejea Santiago Bernabeu.

Mmoja ya wachezaji wanaohusishwa kwenye mikakati hiyo ni Miralem Pjanic.

Kiungo huyo mchezeshaji wa Juventus, raia wa Bosnia, ni aina ya wachezaji wanaoamua kasi ya mchezo uweje awapo uwanjani. Ndiye anayeifanya Bianconeri icheze inavyocheza. Achana na mabao ya akina Cristiano, hapa ndipo roho ya Juve ilipo.

5. Kevin De Bruyne

(Man City)

De Bruyne sio mchezaji bora duniani. Lakini ni fundi hasa. Ni aina ya mchezaji ambaye kila kocha anaona fahari kuwa naye. Ana utundu, akili ya mpira, nguvu, kasi na uwezo mkubwa wa kuongea na mpira ukamsikiliza anachotaka.

Mbelgiji huyu, anaweza kupiga pasi, mashuti, chenga, kuzuia, kukaba, kuachia krosi na kufunga mabao.

4. David Silva

(Man City)

Amekuwa nyota inayoing’arisha Manchester City, tangu alipojiunga nao miaka nane iliyopita. Silva alishinda taji lake la tatu la EPL msimu uliomalizika na sasa anaelekea kubeba ndoo ya tatu, tena akiwa na kitambaa cha unahodha.

Ana uwezo wa kucheza katika wingi ya kulia, kushoto na kati, kama

kiungo mshambuliaji (Namba 10), japo kwa uhalisia ni kiungo wa kati mchezeshaji. Ni mwepesi wa kufanya maamuzi. Licha ya umri wake mkubwa wa miaka 33, Silva bado yuko fiti kila idara.

3. Toni Kroos

(Real Madrid)

Toni Kroos, ndiye anayeendesha mapigo ya moyo wa Real Madrid, kwa sasa. Ndiye anyeamua kasi ya Los Blancos, kuanzia katika kiungo cha kati. Fundi wa kupiga pasi, kufunga mabao na krosi. Nyota huyu wa zamani wa Bayern Munich, ameshindikana!

Ana akili sana, ana uwezo wa kutengeneza nafasi hata pale usipomtegemea. Anajua ni muda gani mechi inatakiwa kuwa na kasi au kwenda taratibu.

2. N’Golo Kante (Chelsea)

Kante (27), ni tofauti na viungo wengine wote katika orodha hii. Ni mmoja wa viungo bora wa kati duniani kwa sasa. Mshindi huyu wa taji la EPL mara mbili na Kombe la Dunia, ndiye Claude Makelele wa zama hizi.

Chini ya Maurizio Sarri, Kante amekabidhiwa majukumu mapya. Anatumika zaidi kushambulia na sio kukaba kama zamani.

Msimu huu, Mfaransa huyu, amefunga mabao na kutoa asisti pia.

1. Luka Modric

(Real Madrid)

Fundi mwenyewe, mshindi wa Ballon d’Or 2018, ni baba lao hasa. Luca Modric (33), ameonesha uwezo mkubwa katika miaka ya hivi karibuni, hususan mwaka jana, ambapo aliiongoza Croatia kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Dunia.

Ndiye malaika aliyetumwa kuvunja utawala wa miaka 10 wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, katika ulimwengu wa soka, kama sio kuutikisa.

Mwaka jana, Modric pia aliisaidia Madrid, kushinda Ligi ya Mabingwa kwa mara tatu mfululizo.