Kisa Simba, Yanga yamsimamisha mwanasheria wao

Muktasari:

Simon alikaimu nafasi hiyo baada ya David Ruhago kufurushiwa virago.

KAMATI ya Utendaji ya Yanga imemsimamisha kazi Kaimu Katibu Mkuu ambaye pia ni  Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama , Wakili Simon Patrick.
Maamuzi hayo yamekuja baada ya kikao cha dharula cha Kamati  ya Utendaji kilichokaa Novemba 17, 2002 jana Jumanne ambacho kilifanyika maalum kwa ajili ya kusikiliza shutuma  ambazo amehusishwa nazo.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Yanga ikisainiwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Dk Mshindo Msola imeeleza kuwa "Dhumuni la kuhakikisha haki inatendeka, kamati ya utendaji itateua  kamati huru kuchunguza suala hili na kutoa maamuzi yenye tija kwa pande zote.
Msola ameongeza kuwa "Kamati ya utendaji itaisubiri kamati huru kukamilisha uchunguzi wake na kutoa ripoti juu ya tuhuma hizi."
Inaelezwa kwamba Simon anatumhumiwa kuwa na ukaribu na baadhi ya viongozi wa Simba hali ambayo imewafanya viongozi wa Simba kuwa na wasiwasi nae.
Hata hivyo jana kupitia ukurasa wake wa Instagram, Simon.esq aliweka orodha ya vitu vitano ambavyo ameweka kama anatuhumiwa navyo.
VIKAO VYA SIRI  NA KIONGOZI  MAASIMU

"Nakiri kukutana na  Mtendaji mwenye rank kama Yangu kama alivyotaja maeneo ya Yatch Club, lakini sio vikao vya siri kwani kilichonikutanisha nae mtendaji huyo ni suala muhimu ambalo viongozi watatu walinituma na baada ya kikao hicho nilirejesha taarifa na hii naongelea ilikuwa Oktoba 20, 2020".
NAHOFIA NAFASI YANGU KUCHUKULIWA NA SENZO

"Mimi nakaiumu nafasi  ya katibu mkuu kwa muda lakini nimeajiriwa kama Mkurugenzi wa Sheria, hivyo basi siwezi kumuhofia Mr Senzo kwani yeye sio mwanasheria bali ni mshauri mkuu wa klabu, kukaimu nafasi maana yake ni unashikiria kwa muda viongozi wanaweza kupiga simu moja tu kwamba kuanzia leo sio kaimu tena na nikatii hofu sijui inatokea wapi.
Masuala mengine aliyoandika ni kuhujumu kesi ya Bernard Morrison, kufuta kesi hiyo Shirikisho la Soka nchini (TFF) na kutopokea simu za Mwenyekiti wake.