Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kilimanjaro Stars yachapwa na Kenya ufunguzi Chalenji

Muktasari:

Kenya ni mabingwa watetezi wa mashindano ya Chalenji wakiwa wamelitwaa taji mwaka 2017 yalipofanyika nchini mwao

Kampala, Uganda. Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' imeanza vibaya mashindano Chalenji baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa mabingwa watetezi Kenya katika mchezo unaochezwa kwenyeUwanja wa KCCA jijini Kampala.

Bao la Kenya lilifungwa na mshambuliaji Abdallah Hassan katika dakika ya tatu ya mchezo na kudumu hadi filimbi ya mwisho. Matokeo hayo Kenya inaongoza Kundi B ikiwa na pointi 3 ikifuatiwa na Sudan na Zanzibar zenye pointi moja kila moja huku Tanzania Bara ya mwisho.

Hassan alifunga bao hilo kwa shuti la chinichini ambalo lilipita kulia kwa kipa Aishi Manula na kujaa wavuni akimalizia pasi ya Oscar Wamalwa.

Ilikuwa ni rahisi kwa Hassan kukwamisha mpira huo nyavuni kwani aliupokea akiwa anamtazama Manula ambaye licha ya juhudi zake kulipunguza lango, mshambuliaji huyo anayechezea Bandari FC ya Kenya aliujaza nyavuni.

Mara baada ya kuingia kwa bao hilo, Stars iliamka na kuanza kumiliki mpira huku ikijaribu kutengeneza mashambulizi ingawa safu ya ulinzi ya Kenya ilikuwa ngumu kupitika.

Changamoto kubwa kwa Stars imekuwa ni kukosa ubunifu wa kupiga mipira ya mwisho kwenda kwenye lango la adui jambo ambalo linaichelewesha kupata bao la kusawazisha.

Hata hivyo pamoja na kutanguliwa kufungwa bao, kikundi cha mashabiki Watanzania wanaoishi nchini hapa kimeendelea kuipa sapoti timu hiyo kwa kushangalia.

Katika dakika ya 22, mwamuzi Ali Sabila wa Uganda, alimuonyesha kadi ya njano mchezaji David Owino wa Kenya kwa kuonyesha utovu wa nidhamu baada ya kulalamikia uamuzi wake

Kipindi cha pili benchi la ufundi Kilimanjaro Stars lilifanya mabadiliko ya kuingia kwa wachezaji Eliuter Mpepo na Ditram Nchimbi, Stars imeonekana kuliweka katika wakati mgumu lango la Kenya tofauti na kipindi cha kwanza.

Katika dakika 45 za kipindi cha kwanza, walinzi wa Kenya walicheza kwa uhuru mkubwa na mara kwa mara walishiriki katika kuanzisha mashambulizi lakini kipindi cha pili wamelazimika kubaki nyuma kwa muda mrefu ili kuwachunga washambuliaji hao.

Mpepo ndiye alianza kuingia katika dakika ya 42 kuchukua nafasi ya Lucas Kikoti na Nchimbi alipishana na Paul Nonga katika dakika ya 63.

Maumbile ya Kikoti na Nchimbi wamekuwa wakiyatumia vyema kukabiliana na mabeki Joash Onyango na Johnstone Omurwa ambao ni warefu kama wao.

Kikosi cha Stars:

Aishi Manula, Mwaita Gereza, Mohamed Hussein, Kelvi Yondani, Bakari Mwamnyeto, Jonas Mkude, Cleoface Mukandala, Mzamiru Yassin, Paul Nonga, Lucas Kikoti na Miraji Athuman