Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kili Stars hasira kwa Wakenya, Uganda walikuwa moto!

Muktasari:

Kilimanjaro Stars ilikutana na Kenya katika hatua ya makundi na kupoteza kwa bao 1-0.

KOCHA wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars', Juma Mgunda amesema kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Uganda kimepita na sasa nguvu yao wanaielekeza katika mchezo wa  kuwania mshindi wa tatu dhidi ya Kenya, utakaopigwa keshokutwa Alhamisi mchana kwenye Uwanja wa KCCA, Uganda.
"Niwapongeze wenzetu Uganda kwa kupata ushindi kwa bao moja halali ambalo halina hata utata. Niseme tu kwamba mashindano bado hayajaisha hivyo tunaenda kujipanga ili tufanye vizuri katika mechi ya kuwania mshindi wa tatu," alisema Mgunda.
Wakati mwenzake Kocha wa Uganda, Jonathan McKinstry alisema ameridhishwa na matokeo waliyopata huku akiipongeza Kilimanjaro Stars:
"Kipindi cha kwanza tulikuwa na nafasi za kumaliza mchezo lakini tulishindwa kufanya hivyo ingawa tuliweza kubadilika kipindi cha pili na kuweza kufunga bao lililotupa ushindi.
 Hata hivyo kama nilivyotabiri mwanzo kuwa mechi hii haitokuwa rahisi na ndivyo ilivyotokea kwani Tanzania Bara walikuwa wagumu na walicheza kwa nidhamu ya hali ya juu ambayo ilituweka katika hatari ya kupoteza mchezo."
Bao la kichwa la dakika za jioni lililofungwa na mshambuliaji wa Uganda, Fahad Bayo katika dakika ya 86, limezima ndoto ya Kilimanjaro Stars kutinga hatua ya fainali ya mashindano ya Chalenji yanayoendelea nchini Uganda.
Udhaifu wa safu ya ulinzi ya Stars ulijionyesha kuanzia kipindi cha kwanza ambapo iliwaruhusu Uganda kupenya kuingia katika lango lao mara kwa mara na ilifanya makosa ya kupoteza mipira, kukosa mawasiliano pamoja na kutokaba.
Ni bahati tu unaweza kusema ndio iliwaokoa Kilimanjaro Stars imalize kipindi cha kwanza ikiwa haijaruhusu bao kwani wenyeji walipoteza nafasi nne za wazi ambazo zingewafanya waweze kufumania nyavu ikiwa wangekuwa na utulivu kupitia kwa Bright Anukani, Allan Okello na Paul Willa.
Hata hivyo katika kipindi cha pili, benchi la ufundi la Uganda lilionekana kubaini udhaifu wa Stars na kuamua kubadili mbinu jambo ambalo liliisaidia kupata ushindi katika mchezo huo.
Uganda badala ya kupiga pasi fupifupi za haraka kama ambavyo walifanya mwanzoni, walitumia mbinu za kupiga krosi ambayo ilionekana kuwapa tabu walinzi wa Stars katika kuziokoa.
Mbinu hiyo ndio iliwapa bao pekee lililoamua mchezo baada ya Kizza kupiga krosi hiyo na kumkuta Bayo ambaye aliruka akiwa huru na kuujaza wavuni mpira huo.
Kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza ambapo Stars mara kadhaa ilijibu mashambulizi hayo ya Uganda, hali ilikuwa hivyo katika kipindi cha pili lakini hata hivyo haikuweza kubadili ubao wa matokeo.
Stars ilijaribu kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Nickson Kibabage na Eliuter Mpepo na nafasi zao kuchukuliwa na Cleoface Mkandala na Paul Nonga lakini hawakuweza kuiokoa.
Kipindi hicho cha pili, refa Diraneh Gueidi kutoka Djibout aliwaonyesha kadi za njano Mzamiru Yassin, Gadiel Michael na Kelvin Yondani kutokana na rafu walizocheza kwa wachezaji wa Uganda na pia utovu wa nidhamu.
Kwa upande wa Uganda, aliyeonyeshwa kadi ya njano alikuwa ni kiungo Joackim Ojera ambaye alimfanyia madhambi kipa, Metacha Mnata.
Katika hali ya kushangaza, mwamuzi Gueidi alizua mshangao mnamo dakika ya 68 baada ya kuizawadia Uganda penati akidai Abdulkarim Watambala aliangushwa ndani ya eneo la hatari la Stars ingawa baadaye alibatilisha uamuzi huo.
Mwamuzi msaidizi kutoka Somalia, Omar Abdoulkadir alichangia kwa kiasi kikubwa kubatilishwa kwa uamuzi huo kwani aligoma kuelekea katika boksi la Kilimanjaro Stars na badala yake akaamua kubaki katika eneo lake.
Baada ya majadiliano mafupi baina ya Gueidi na msaidizi wake, uamuzi huo ulibadilika na refa huyo kuamuru pigo la faulo ambalo halikutumiwa vyema na Uganda kupata bao.
Ushindi huo umeifanya Uganda kuungana na Eritrea kutinga hatua ya fainali ambayo itachezwa kesho Alhamisi wakati Kilimanjaro Stars itakabiliana na Kenya katika mechi ya kuwania mshindi wa tatu ambayo nayo itachezwa Alhamisi mchana katika uwanja ambao itapigwa pia fainali wa KCCA.
Eritrea walitinga fainali baada ya kuichapa Kenya kwa mabao 4-1 katika mchezo wa utangulizi uliochezwa uwanjani hapo leo mchana kabla ya mechi ya Kilimanjaro Stars na Uganda.
Mabao mawili ya Abel Okbay, moja la nahodha Robel Teklemichael na lile la kujifunga la Oscar Wamalwa yalitosha kuifanya Eritrea iandike historia ya kutinga fainali ya mashindano hayo kwa mara ya kwanza.
Bao pekee la kufutia machozi kwa Kenya lilifungwa na Wamalwa huyohuyo katika dakika ya 53