Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikosi kipya Yanga chaibua fomesheni mpya

Fred Minziro,Kocha msaidizi wa Yanga

MICHAEL MOMBURI YANGA imeangalia usajili wa Simba na Azam ikacheka, lakini imetamka kwamba inakuja kwa kishindo na fomesheni ya kutisha msimu ujao, ambayo itaifanya itambe kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Benchi la ufundi la timu hiyo limetamka maneno hayo kwa kujiamini na kusisitiza kuwa usajili lililoufanya ni sahihi na wala hawajaingiliwa kwa namna yoyote ile na anayebisha asubiri uwanjani aone mambo. Kocha Msaidizi Fred Minziro amesema usajili wao haukuangalia majina bali uliangalia uwezo binafsi na mapengo yaliyokuwa kikosini msimu uliopita. Alisema usajili huo si wa kiholela kwa kuwafurahisha baadhi ya watu, ndiyo maana wamesajili majina mawili kila nafasi. "Tumesajili kikosi cha bandika bandua, kikosi cha watu wa kazi wala hatujasajili mtu kwa fasheni. Kila nafasi ina vichwa viwili au zaidi na mtu akizubaa atakuwa kwenye wakati mgumu sana na hatutakuwa na huruma naye," alisema Minziro na kusisitiza kuwa wana uwezo wa kutumia fomesheni yoyote wanayoitaka. "Tumesajili kwa kuangalia mashindano yanayotukabili, kila mchezaji aliyesajiliwa ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja na ndiyo aina ya timu tuliyokuwa tunaitafuta. "Msimu uliopita tuliichukua timu sehemu mbaya sana, unamlazimisha mpaka beki kucheza kama mshambuliaji, ilikuwa hatari sana, sasa tumeamua kufanya usajili wa maana. "Tulijua kwamba Simba, Azam na nyingine zitajipanga vizuri na Ligi itakuwa kali zaidi ya zote zilizowahi kuonekana miaka ya nyuma, wala hatutishiki na wachezaji wenye majina waliosajiliwa na wapinzani wetu, unaweza kukusanya wachezaji wa kila aina lakini wasipojituma ni kazi bure, soka ni uwezo si umaarufu. "Hatutaki mchezaji legelege, tukianza mazoezi Juni 21 ni mchakamchaka kwenda mbele, tunataka timu iwe imara tuingie kwenye mashindano tukiwa fiti tofauti na kipindi cha nyuma, mtu mvivu atapata shida tumeandaa programu nzito," alisema beki huyo wa zamani wa Yanga aliyewahi kuzinoa JKT Ruvu, Prisons na Moro United. Minziro, ambaye sasa anafanya kazi ya kuisuka timu ya vijana ya Yanga, alisisitiza; "Tunataka timu icheze mpira wa kushambulia, kuvutia na ushindi upatikane kadiri inavyohitajika, tumejizatiti idara zote, mbele palikuwa pamelegea tumekaza kama tulivyofanya kwenye idara nyingine. "Tumeongeza wachezaji watatu wapya wa kigeni na wengine kama nane hivi wa humu ndani, ambao wote ni watu wa kazi, kikosi kitakuwa na wachezaji kama 28." Kocha huyo pia aliwaponda baadhi ya wadau wanaokosoa usajili wa Yanga; "Nashangaa sana unazungumzia Yanga wakati huijui na si kazi yako? Tuache fitina, tuachieni timu yetu, sisi ndio tunaojua na tuna mamlaka ya kusajili na tumeshasajili, subirini uwanjani, mbona hamkosoi timu nyingine?" Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wake wa Kamati ya Usajili, Salum Rupia imetangaza kuwasajili makipa Shabaan Kado (Mtibwa) na Said Mohammed (Majimaji), winga Julius Mrope (Mtibwa), mabeki David Luhende(Kagera), Oscar Joshua (Moro United), Godfrey Taita(Kagera) na Tonny Ndollo (Kagera). Wengine ni viraka Pius Kisambale (JKT Ruvu), Rashid Gumbo (Simba) wakati Haruna Niyonzima (APR-Rwanda) na Kenneth Asamoah (Ghana) wako katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wao. Katika majina hayo, ukiondoa makipa wawili Kado na Said, wachezaji wengine kila mmoja anachezea nafasi zaidi ya moja uwanjani.