Kigogo amkingia kifua kocha Milan

Muktasari:

  • Milan ni bingwa mara saba wa Ligi ya Mabingwa Ulaya

Milan, Italia. Mtendaji Mkuu wa AC Milan, Marco Fassone amesema kibarua cha kocha wa timu hiyo, Vincenzo Montella kipo salama.

Kauli ya Fassone imekuja muda mfupi baada ya AC Milan kuchapwa mabao 3-2 na watani wao wa jadi Inter Milan katika mchezo wa Ligi Kuu Italia juzi usiku.

Baada ya kipigo, ziliibuka tetesi kuwa kocha huyo anaweza kutupiwa virago muda mfupi ujao, lakini bosi wake amekanusha uvumi huo.

Matokeo hayo yamemuweka katika mazingira magumu kocha huyo wa zamani wa Sampdoria. AC Milan inashika ipo nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi Kuu Italia.

"Tutakuwa na Montella anahitaji kupewa muda wa kufanya kazi, jambo la msingi ni kumuunga mkono na kumpa ushirikiano," alisema Fassone.